Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa amesema changamoto zinazowakabili wakazi wa kata
ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga atazifikisha sehemu husika ili ziwezi
kushughulikiwa.
Ametoa ahadi hiyo leo Jumatatu Juni 19,2023 wakati
akizungumza na wakazi wa kata ya Ngokolo kwenye mkutano wake wa hadhara ambapo
baadhi ya wananchi wametaja changamoto ikiwemo changamoto ya miundombinu ya
barabara.
Baadhi ya wananchi wamelalamikia ucheleweshwaji wa
fedha za TASAF baada ya utekelezaji wa miradi na kwamba wamedai kutolipwa Miezi
minne ambapo wamemuomba mwenyekiti huyo kufuatilia changamoto hiyo ili waweze
kupata pesa zao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa
ameahidi kufuatilia kero zinazowakabili huku
akiwaomba wananchi hao kuwa wavumilivu wakati changamoto hizo zinatafutiwa
ufumbuzi.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga amewaomba
wakazi wa kata ya Ngokolo kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita
chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwa na maendeleo endelevu.
Aidha amewapongeza viongozi mbalimbali wanaosimamia miradi katika Manispaa ya Shinyanga na kwamba amewaomba wakazi wa kata ya Ngokolo kuendelea kushirikiana na viongozi wa chama na serikali akiwemo diwani wa kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko pamoja na Mbunge wa jimbo la Shinyanga ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana na ajira Mhe. Paschal Parobas Katambi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa
Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza na wakazi wa kata ya Ngokolo kwenye
mkutano wa hadhara leo Jumatatu Juni 19,2023.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza na wakazi wa kata ya Ngokolo kwenye mkutano wa hadhara leo Jumatatu Juni 19,2023.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akimpongeza diwani wa kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu kulia leo leo Jumatatu Juni 19,2023 kwenye mkutano wa hadhara.
Mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, ukiendelea katika kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Juni 19,2023

Mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, ukiendelea katika kata ya Ngokolo
Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Juni 19,2023
Mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, ukiendelea katika kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Juni 19,2023
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioratibiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, kwa lengo la kuzungumza na kupokea kero za wakazi wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Juni 19,2023.