DC SAMIZI, KAMANDA MAGOMI WAIPONGEZA SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ameipongeza kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa juhudi mbalimbali wanazozifanya katika kupinga ukatili.

Ametoa pongezi hizo leo Julai mosi Mwaka 2023 akiwa mgeni rasmi kwenye bonanza la kataa uhalifu toa taarifa, ambao limefanyika katika kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.

DC Samizi amesema SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wamekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukatili kwa kuibua pamoja na kutoa elimu ya ukatili katika sehemu mbalimbali na kwamba amesema serikali inatambua mchango wao.

Amewasihi viongozi na wanachama wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kuendelea na juhudi hizo za kupambana na ukatili unaoendelea kwenye familia na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi naye pamoja na mambo mengine ameipongeza kampeni ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kuisaidia serikali katika hatua za kutokomeza vitendo vya ukatili Mkoani Shinyanga.

Kamanda Magomi ameahidi kuendelea kushirikiana na SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga katika utekelezaji wa majukumu ili kuimarisha usalama hasa kwa wanawake na watoto.

Akizungumza Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi kampeni hiyo itaendelea kushirikiana na viongozi wengine wanaotetea haki na kwamba amesema wataendelea kutoe elimu kwenye jamii ili iweze kufahamu madhara ya ukatili.

Madam Kisendi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa za viashiria pamoja na vitendo vya ukatili ili hatua zaidi ziweze kuchukulia na mamlaka husika.

Kampeni ya SMAUJATA imeanzishwa Mwaka jana na Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa Bwana Sospeter Bulugu ikiwa lengo ni kuisaidia serikali kutokomeza ukatili Nchini.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi akiipongeza SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga leo Julai mosi Mwaka 2023 katika bonanza la kata uhalifu toa taarifa.

  

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakishirikia leo kwenye bonanza la kataa uhalifu toa taarifa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.






This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post