Spika wa Tanzania aelezea malengo ya mkutano wa SADC.

 

Na Jane Edward,Arusha 


SPIKA  wa bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Tulia Akson amesema kuwa ,Mabunge   ya Jumuiya  ya  Maendeleo Kusini   mwa Afrika  wamekusanyika  jijini Arusha kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo  maswala ya kilimo.


Ameyasema hayo jijini Arusha kwenye  kikao cha 53 cha jukwaa la  Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinacholenga kujadili usalama wa chakula na tatizo la ajira kwa vijana.




"Hiki ni   kikao cha 54 na ni mara ya nne kufanyika hapa nchini Tanzania  kukusanya mabunge haya tunataka kuhakikisha Tanzania na jumuiya ya nchi za Afrika inajitosheleza  kwa chakula."amesema Dk.Tulia.


Amesema ,wanataka kuona vijana wengi wanajiwekeza katika eneo hilo na kuhakikisha wanajiajiri katika sekta hiyo ya kilimo kwani ni sekta ambayo inaajiri  idadi kubwa ya watanzania .


Ameongeza kuwa, sasa hivi  nchi ya Tanzania  imeanza kupiga hatua na fedha nyingi zimewekezwa  katika eneo hilo na wadau mbalimbali  kujitokeza kuwekeza katika sekta hiyo lengo likiwa ni  kuhakikisha  kuna uwekezaji  wa kutosha  katika  sekta hiyo.


Amesema ,kwa sasa hivi  Tanzania wanafanya vizuri sana na  wanaweza kulisha Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. 


Mkutano huo wa siku Saba unashirikisha wabunge wa SADC kutoka Zimbabwe,Namibia,Sherisheri,Afrika Kusini, Lesotho,Malawi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Eswatini,Angola, Botswana,Zambia, na wenyeji Tanzania.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post