CAG awafunda Wanahabari Arusha

 

Valence Rutakyamirwa, mwakilishi wa mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Arusha 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amewataka Waandishi wa Habari kutenga muda wa kutosha kusoma taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za taasisi za Serikali zinazotolewa na ofisi yake  ili kuwawezesha  kutoa taarifa sahihi na za ukweli kwa jamii.

Hayo yameelezwa leo Agosti 28,2023 na Mwakilishi wa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa Nje (CEA) Mkoa wa Arusha, Valence Rutakyamirwa katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha.

Rutakyamirwa amesema mafunzo hayo yametolewa kwa lengo la kuwajengea waandishi wa habari uwezo wa kutafuta na kuripoti kwa usahihi taarifa za ukaguzi na udhibiti wa fedha za umma  ikiwemo sheria, kuichambua ripoti na misingi ya mawasiliano baina ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Vyama vya Waandishi wa Habari.

"Ofisi ya CAG imeamua  kuwajengea Waandishi wa Habari  uelewa juu ya mbinu za kutambua aina za ripoti za ukaguzi, Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ili kuwawezesha kuripoti taarifa sahihi kwa jamii kuhusu matumizi ya  fedha za umma,"amesema.

Kwa upande wake Msaidizi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kitengo Cha Huduma za Kiufundi (TSSU),Deogratisu Kirama amesititiza kuwa ofisi hiyo imeajiri wataalam wa kutosha ili kuleta tija zaidi katika ukaguzi na udhibiti wa fedha za umma.

"Katika kudhibiti matumizi sahihi ya fedha za Umma Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) inawataalaam wabobezi 400 Wenye CPA ikiwemo wataalam wengine wenye taaluma mbalimbali nchini."

Pia amesema ni vema wanahabari wanaochambua na kuandika taarifa za CAG kujua aina za matumizi ya fedha za umma au za miradi na  zimefanya kazi gani. 

Amesema katika miradi kuna  miradi mingi isiyotekelezwa hivyo ni jukumu la Mwandishi kuwa makini wakati wa kuchambua na hata kama kuna hati safi imetolewa bado ukienda chini kuna kasoro za sheria ya bajeti na manunuzi na hapo utaweza kubaini kasoro zilizopo.

"CAG ameajiri wataalam wengi ikiwemo wenye CPA ili kuleta tija zaidi katika kaguzi lakini pia tunafanya ukaguzi wa kifanisi ambao ni wenye tija na ufanisi katika maeneo yaliyochaguliwa na sio kwa kila  taasisi "

Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Elieshi Saidimu amewataka wanahabari kuandika zaidi taarifa zinazotolewa na CAG ikiwemo kujua sheria,kanuni na taratibu zinazoratibu uendeshaji wa ofisi hiyo sanjari na kuchambua taarifa zinazotolewa na CAG.

Mwenyekiti wa Arusha Press Club Claud Gwandu akizungumza wakati wa ufunguzi
Washiriki wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa




IMMANUEL MSUMBA Managing Director mobilePhone +255 762 561 399 emailAddress Msumbanews@gmail.com website https://www.msumbanews.co.tz/

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post