Daladala zagoma tena Arusha, huku Afisa Latra akihamishwa ghafla

Abiria wakiwa wamepanda gari za mizigo kwenda kwenye shughuli za kila siku ndani na nje ya Jiji la Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha 

Migomo ya daladala na bajaji inayoendelea bila kupatiwa ufumbuzi katika jiji la Arusha,imetajwa kumng'oa aliyekuwa ofisa mwandamizi wa Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini (LATRA) mkoa wa Arusha Amani Mwakalebela baada ya kushindwa kutatua migogoro hiyo na kusababisha usumbufu kwa wananchi ,wafanyabiashara na wanafunzi kukosa usafiri.

Mwakalebela amepata uhamisho wa  ghafla wakati bado sakata la mgomo wa daladala halijapoa huku mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akiwa ameunda kamati ya usuluhishi juu ya mgogoro  huo na kuja na majibu.

Leo jumatatu Agosti 14, 2023 wakati ofisa mpya Mwandamizi wa LATRA Joseph Maiko akitinga ofisini kwake rasmi kuchukua nafasi ya Mwakalebela, daladala zimegoma tena na kusababisha adha kwa wananchi.

Akiongea  na vyombo vya habari ,Maiko aliwataka wamiliki wa daladala katika jiji la Arusha, kusitisha mgomo wao mara moja na kurejesha usafirishaji kwa kuwa mamlaka hiyo imeanza kutekeleza maoni ya kamati iliyoundwa na mkuu wa mkoa .

Alisema iwapo daladala zitaendelea na msimamo wakutotii mamlaka ya kuwataka wasitishe mgono mara moja,LATRA itafuta leseni zao mara moja kama sheria inavyotaka.

"Mimi nimeingia ofisini Leo jana tulikutana na viongozi wa vyombo vya usafirishaji kwa lengo la kujitambulisha kama afisa mpya wa LATRA Arusha, na Leo nimejaribu kuzungukia baadhi ya maeneo ikiwemo ruti za daladala zaidi ya 145 ,mimi na wenzangu tupo katika hatua ya kutekeleza maoni ya kamati hiyo "

Kuhusu ofisa aliyekuwepo kuondolewa  ghafla katika kituo chake cha kazi mkoani Arusha, alisema ni uhamisho wa kawaida haihusiani na mgogoro wa daladala na bajaj. 

Mgomo wa daladala umerudia tena leo jijini hapa, huku madereva wa magari hayo wakimwomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati mgogoro uliopo kati yao na madereva wa pikipiki za matairi matatu maarufu kwa jina la Bajaj.

Mgomo huo unafanyika leo Agost 14 ikiwa ni mara ya tatu mfululizo, ukiwemo mgomo uliofanyika Julai Mosi na mwingine ukafuatia wa Julai 3 mwaka huu, ambapo madereva daladala wamekuwa wakishinikiza kuondolewa kwa usafiri wa bajaji katika barabara wanazohudumu kwani zinawanyima biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, mmoja wa madereva daladala Herman Elias alisema katika mgomo wao wa pili, Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela aliitisha kikao cha madereva hao na kusikiliza madai ya daladala na Bajaji na kuahidi kuchukua hatua ya utatuzi.

Aidha mgomo huo unadaiwa kuchangiwa pia na kupanda kwa nishati ya mafuta ambapo hivi sasa petroli inaumizwa kwa Tsh3283 kwa Jiji la Arusha

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post