Internet kutolewa Bure kwa jamii: Serikali

Na Seif Mangwangi, Arusha

HUENDA kampuni za Simu nchini zitapunguza mapato yake kwa kiwango kikubwa kufuatia hatua ya Serikali kuendelea kukamilisha miundo mbinu yake ya Internet na kuanza kutoa huduma hiyo bure kupitia mfumo wa WiFi.


Akizungumza jana jijini Arusha, Naibu Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Methew  Kundo, wakati akifungua kikao cha 41 cha Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kinachoendelea Jijini hapa.


Mhandisi kundo amesema Serikali inajipanga kuimarisha huduma za mawasiliano nchini, kwa kuweka mtandao wa Intaneti wa bure  (WiFI) kwenye mikusanyiko yote, vyombo vya usafiri na kwenye shule, ili kila mwananchi apate huduma hiyo bila usumbufu wowote


Akizungumzia mkutano huo, Mhandisi Kundo amesema kikao hicho, kimefanyika ikiwa ni mfululizo wa vikao vyao, kwa ajili ya kuandaa ajenda ya pamoja kwa nchi za Afrika, ili kuziwasilisha  katika kikao cha Baraza la Posta Duniani kitakachofanyika Oktoba mwaka huu.


Amesema uwekaji huo wa Intaneti za bure, zitasaidia wananchi kupata huduma za mawasiliano popote wanapokuwa na kuendelea na shughuli zao za kijamii, bila mkwamo wa ukosefu wa huduma hiyo.


“Serikali ya awamu ya sita imejipanga, tunataka kuhakikisha umoja huu na wenzetu unaboresha  mifumo ya utendaji kazi na kua ya kidijitali na sisi kama Tanzania  tukiwa wanachama wa umoja huu  Afrika na Duniani, tumeanza mikakati,"amesema.


Amesema miongoni mwa makubaliano yaliyowekwa na Umoja wa Posta Afrika ni pamoja na kuboresha miundo mbinu yetu ya Mawasiliano kwa kuweka sawa  sera yetu ya posta ya mwaka 2003, ”amesema


Amesema mojawapo ya maboresho hayo ni  ujenzi wa minara, mkongo wa Taifa na uwekaji wa Anuani za Makazi, ili kuhakikisha  shughuli zote za posta zinafanyika vizuri na wananchi wanapata huduma za kijamii bila usumbufu.


Aidha, amesema Rais Samia Hassan Suluhu  mwaka jana Februari 8  alihakikisha Tanzania kunakua na Anwani za makazi na hilo lilifanyika kwa ufanisi, ambapo kwa sasa kila mmoja anaona faida yake katika upatikanaji wahuduma za kijamii na hata posta inakua rahisi.

“Tunavyoelekea kutoa huduma zote kidijitali ni lazima kuhakikisha uwezo wetu kimtandao unakua imara  ili ifike mahali, kila mmoja asione umuhimu wa kutembea na fedha tasilimu, bali kadi tu na kupata kila aina ya huduma mtu anayohitaji kupata,”amesema


Awali Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la PAPU, Richard Ranarison, amesema umoja huo unakusudia kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kila nchi na ili kufikia lengo hilo,  kila wanapokutana kwenye vikao vyao vya kila mwaka wanaangalia wapi walipo na wanapoelekea na penye dosari wanazirekebisha.



This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post