MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA NA LAKI TANO YAPITISHWA NA MWENGE WA UHURU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu (mwenye scalf) alipokuwa kwenye mapokezi ya mwenge wa Uhuru, kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kasulu Abdallah Mbelwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Eliah Kagoma.

minane iliyotembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, anaripoti Respice Swetu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya

halmashaurti ya wilaya ya Kasulu na mji wa Kasulu kwenye eneo la Nyumbigwa

mjini Kasulu, kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2023  Abdallah

Kaim, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa kazi nzuri ya kusimamia

utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopitiwa na mwenge huo na

kuifanya halmashauri hiyo kukamilisha mbio na hati safi.

 “Nichukue nafasi hii kumpongeza sana mkuu wa wilaya ya

Kasulu Kanali Isack Mwakisu, mkurugenzi, madiwani, Chama cha Mapinduzi, wakuu

wa idara, vitengo pamoja na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu kwa

kazi iliyotukuka, tumeoina miradi katika maeneo mbalimbali tuliyopita na

kuridhika nayo, nami kwa dhati kabisa niseme kuwa halmashauri ya wilaya ya

Kasulu mmeupiga mwingi”, alisema.  

Aliongeza pia kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi

shupavu wa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitoa pesa nyingi kwa ajili ya

kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi hivyo ni jambo la faraja kuona kuwa

pesa hizo mmezisimamia ipasavyo.   

Awali baada ya mapokezi yaliyofanyika katika kijiji cha Mvugwe,

mwenge wa uhuru ulianza mbio zake kwa kuzindua majengo ya vyumba viwili vya

madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi ya Kumganza mradi

uliotekelezwa kwa thamani ya shilingi 80,750,000 kupitia ufadhili wa World

Vision.

Miradi mingine iliyotembelewa na mbio za mwenge wa uhuru na

thamani ya miradi hiyo ikiwa kwenye mabano ni pamoja  kikundi cha

waendesha bodaboda wa kijiji cha Makere (40,000,000/=), mradi wa bustani ya

kuzalisha miche ya miti katika kijiji cha Kalimangoma (250,000,000/=) na mradi

wa maji safi na salama kwenye kijiji cha Mkesha (253,400,272/=).

AIidha katika eneo la hospitali ya halmashauri ya wilaya ya

Kasulu, kiongozi wa mwenge wa uhuru aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa

nyumba nne za watumishi wa hospitali hiyo (460,000,000/=) na katika ujenzi wa

barabara yenye urefu wa nusu kilometa inayotengenezwa kwa kiwango cha rami

kuelekea katika hospitali hiyo (500,000,000/=).  

Kabla ya kufika kwenye eneo la mkesha, msafara wa mbio za mwenge

wa uhuru ulizindua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya sekondari ya

Rungwampya.

Sanjari na kuzindua, kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya

maendeleo, mwenge wa uhuru umekuwa ukitoa ujumbe wenye kauli mbiu ya kupiga

vita uharibifu wa mazingira, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na kujikinga

na maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post