Wawekezaji wazawa wafurika Kituo Cha uwekezaji

 Wawekezaji wazawa wafurika Kituo Cha uwekezaji

* Hadi Juni 2023 Miradi 129  ya Dola mil1007.67 imeshasajiliwa 


Na Seif Mangwangi, Arusha


Mabadiliko ya sheria mpya ya uwekezaji nchini yameshaanza kuleta matokeo chanya ambapo katika Kipindi cha robo ya pili ya mwaka huu,  Aprili hadi Juni 2023 Kituo cha uwekezaji nchini (TIC),  kimefanikiwa kusajili miradi 129  yenye thamani ya Dola Milioni 1007.67.


Miradi hii inatarajiwa kuzalisha ajira mpya 14,631 kulinganisha na kipindi kama  hicho cha mwaka jana ambapo TIC ilisajili miradi 68 pekee yenye thamani ya dola milioni 478.61 ambayo ilitarajiwa kuzalisha ajira mpya 6474.


Kwa mujibu wa Meneja wa TIC Kanda ya Kaskazini na takwimu zilizopo kwenye jarida linalochapishwa na Kituo hicho,  sekta ya viwanda ilionekana kuongoza kwenye uwekezaji dhidi ya sekta zingine ambapo kwa kipindi hicho miradi 56 ilisajiliwa. Miradi iliyofuatia kusajiliwa kwa wingi katika Kipindi hicho ni kutoka katika sekta za uchukuzi na ujenzi wa kibiashara.


" Ukisoma takwimu katika miradi 56 iliyosajiliwa tunatarajia  nafasi za kazi 7,266 zitatolewa huku miradi hiyo ikiwa na  mtaji unaokadiriwa kufikia dola milioni 465.82," amesema Veronica.


Aidha takwimu za umiliki wa miradi kwa kipindi hicho zinaonyesha kila upande kufanya vizuri ambapo wazawa waliendelea kuhamasika kujisajili kwa wingi, miradi ya pamoja ya wazawa na wageni na miradi ya wageni pekee pia iliongezeka.


"Miradi ya wawekezaji wa nje pekee iliongezeka kwa asilimia 55 kwa kipindi Cha robo ya pili tofauti na mwaka Jana ambapo miradi 28 pekee ilirekodiwa, miradi ya ushirikiano ilifikia32 tofauti na 20 mwaka Jana huku miradi ya wazawa ilifikia 42 tofauti na mwaka Jana ambayo Ilikuwa miradi 20 pekee,".


Kwa mujibu wa Meneja wa Kituo cha uwekezaji Kanda ya Kaskazini, Veronica Mrema amesema mafanikio hayo yanatokana na  sheria mpya ambayo  imetoa unafuu kwa wawekezaji kupata msamaha wa Kodi kwenye miradi ya ukarabati na uboreshaji ambapo mwekezaji anaweza kupewa msamaha wa Kodi kwa kipindi kisichopungua hadi miaka3.


Amesema Kituo Cha TIC kimeendelea kutoa semina na uhamasishaji wa wawekezaji kusajili miradi yao katika Kituo Cha uwekezaji ili waweze kupata unafuu wa kuiendeleza .


Veronica amesema mfano kiwango cha usajili wa Miradi TIC kimepunguzwa kupitia sheria mpya ambapo hivi sasa wazawa wenye miradi ya Dola 50,000 wanaweza kujisajili. Awali sheria ilikuwa inataka ili uweze kujisajili na Kituo hicho ni lazima uwe na mtaji wa kuanzia dola100,000

Ametoa wito kwa Wawekezaji kufika kwenye viwanja vya nane nane kote nchini ambapo wataalam wa kituo Cha uwekezaji watakuwepo kwaajili ya kuwapatia elimu ya uwekezaji na namna wataweza kupata faida baada ya kujisajili na Kituo hicho kwa lengo la kukuza na kupanua biashara zao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post