DC KISSA AFUNGUA MILANGO KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA USAFIRISHAJI NJOMBE ILI KURAHISHA BIASHARA YA MAZAO YA KILIMO KWENDA SOKONI

 NJOMBE , Tanzania 

Mkuu wa wilaya ya Njombe mkoani Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amesema milango ya uwekezaji imezidi kufunguka baada ya kumiminika kwa wawekezaji katika sekta ya mbalimbali ikiwemo usafirishaji na Kilimo jambo ambalo linakwenda kutengeneza fursa ya ajira nyingi kwa vijana na mapato ya serikali.


Hayo yamebainishwa wakati wa uzinduzi wa ofisi za kampuni ya ABC mjini Njombe ambapo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Kissa amesema ujio wa wawekezaji wilayani humo umetokana na mazingira rafiki pamoja na  hamasa ya muda ya mrefu kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo hususani parachichi na kisha kuendelea kualika wawekezaji wengine wa ndani na nje kuja wilayani humo kwa kuwa kuna utajiri wa ardhi yenye rutuba.

Aidha Kissa amesema kupitia mradi huo ,Vijana wanakwenda kupata ajira huku pia akiomba muwekezaji huyo wa sekta ya usafirishaji wa ardhini kuona namna ya kujenga jengo ambalo litatumika kutoa huduma ya chakula kwa abiria.

"Nitoe wito kwa wawekezaji wengine kuja Njombe kuwekeza na milango iko wazi na kwasababu biashara ya usafirishaji ni huria,alisema Kissa Kasongwa DC NJOMBE .<
/span>

Amefafanua kuwa"Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliagiza sisi wawakilishi wake kubuni vyanzo vingi vya mapato na ujio nwa mradi huu wa ofisi ya ABC ni kimoja wapo hivyo tunaendelea kukaribisha wawekezaji wengine wa ndani na nje ya njombe kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali kwa kuwa njombe ina ardhi ya kutosha kwa wawekezaji,Ofisi hii ni ya kisasa na nitoe wito kwa wana Njombe kuja kupiga hata picha ,amesema Kissa Kasongwa Dc Njombe "

Akieleza kuhusu utekelezaji wa mradi huo mkurugenzi wa kampuni ya ABC Severine Ngallo anasema licha ya kupitia changamoto lukuki katika huduma kampuni hiyo imekuwa ikitoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwa zaidi ya miaka 30 na kisha kuwatoa hofu wakazi wa Njombe juu ya ubora wa huduma zinazokwenda kutolewa katika mradi wa ofisi yao mpya iliyogharimu zaidi ya mil 100 hadi kukamilika kwake.

Akiweka bayana sababu ya kuivutia kampuni kuja kuwekeza Njombe Ngallo amesema ni kutokana kasi ya mwingiliano mkubwa wa watu unaosababishwa na uwepo wa fursa nyingi za uchumi ikiwemo ya ya kilimo cha parachichi na mazao mengine ya biashara na kwamba kupia mradi huo serikali inakwenda kupata kodi na vijana kupata ujira wao.

Mbali na kuzungumzia sababu na faida za kuwekeza Njombe lakini pia mkurugenzi huyo amebainisha changamoto zinazowakwamisha katika sekta ya usafirishaji ikiwemo ya kusimamiwa na wizara zaidi ya tano ambazo kila moja ina tozo na sheria zake zinazodhibiti msafirishaji kitendo ambacho kinawafanya wawekezaji wengi kushindwa kutekeza ipasavyo hivyo tunaomba serikali kuitazama kwa jicho la huruma sekta hiyo nyeti.

"Katika sekta hii tinafanya kazi na wizara tano ,Wizara ya uchukuzi,Wizara ya habari na wasiliano, Wizara ya Ujenzi,Wizara ya tamisemi na Wizara ya mambo ya ndani kwa maana ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ambazo kila wizara ina sheria zake na faini mbalimbali ambazo wawekezaji wengi wanashindwa kutekeleza ipasavyo jambo linalosababisha kuifanya kuwa biashara ya kurithishana hivyo tunaomba uingalie kwa jicho la huruma".amesema Ngallo .

Kwa upande wa mwakilishi wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Masoud Kwileka ambaye ni mkuu wa polisi wilaya ya Njombe anasema ujio wa muwekezaji mpya katika sekta ya usafiri wa ardhini mjini Njombe unakwenda kufungua fursa za ajira kwa vijana na kudhibiti vishoka wanaokatisha tiketi na kuwaibia abiria .

Katika hatua ngingine Kwileka ametumia fursa hiyo kumkumbusha muwekezaji huyo kuzingatia sheria za barabarani kwa ajili ya usalama wa abairia na mizigo yao.
 
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Merickzedeck Kaberege amesema halmashauri ilitoa fursa ya muwekezaji huyo kwasababu anakwenda kuchochea ukuaji wa fursa nyingine za uchumi na kisha kuwataka wawekezaji wengine kuja kuwekeza. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post