MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI MASIJARA YA SHINYANGA IMEENDELEA KUSIKILIZA KESI YA UGAIDI

 

Na Moshi Ndugulile

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi shauri namba 3 la Mwaka 2023 inayosikilizwa na Mahakama kuu ya Tanzania masjala ya Shinyanga, wameweka pingamizi la kisheria dhidi ya Jamhuri baada ya  maelezo ya onyo ya mshtakiwa kuchukuliwa kinyume cha sheria,kifungu cha 58.

Mawakili wasomi wa upande wa utetezi kwa pamoja mbele ya jaji Geofrey Isaya wameiomba mahakama hiyo  isiyapokee maelezo ya onyo ya mshitakiwa wa pili kama kielelezo Mahakamani hapo

Mbele ya jaji Geofrey Isaya wakili msomi Shaaban Mvungi anayemtetea  mshitakiwa wa pili, amesema kwa mujibu wa shahidi wa 7 wa jamhuri alimchukua maelezo mtuhumiwa chini ya kifungu cha 58 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai namba 20,iliyofanyiwa marejeo Mwaka 2022, ambapo hata hivyo mshtakiwa hakuanzisha yeye mchakato wa kuchukuliwa maelezo

Mvungi ameiambia mahakama hiyo kuwa licha ya shahidi huyo kuieleza mahakama kwamba alichukua maelezo chini ya kifungu cha 58 lakini kuna makosa mengine katika maelezo ya onyo kwa mujibu wa sheria kifungu cha 57 kifungu kidogo cha 2 aya D,kwamba  mtuhumiwa anapochukuliwa maelezo ni lazima apewe onyo na kuandikwa maelezo,lakini katika onyo hilo haikuonyesha muda wa kutolewa onyo kwa mtuhumiwa

Hata hivyo Wakili Msomi Mvungi amefafanua zaidi kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 50 maelezo hayo yalikuwa nje ya muda

Kwa upande wake wakili wa serikali mwandamizi Jenethreza kitaly mbele ya jaji Geofrey Isaya amesema pingamizi la upande wa utetezi halina mashiko kwa sababu mtuhumiwa alikubali kuchukuliwa maelezo kwa hiyari yake mwenyewe,na kwamba maelezo ya onyo yapo ndani ya muda hivyo ameiomba maakama hiyo kuyapokea maelezo ya onyo kama kielelezo.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo leo septemba 14,2023 shahidi wa 7 amesema Januari 19,Mwaka 2018 mshitakiwa wa pili Hussein Juma alitoa maelezo ya onyo na kukiri kuhusika na vitendo vya kigaidi

Shahidi huyo ameiomba mahakama hiyo  iyapokee maelezo hayo ya mshitakiwa wa pili kama kielelezo kwa kuwa aliyaandika chini ya kifungu cha 58 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022

Mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi masjala ya Shinyanga imeendelea kusikiliza kesi ya ugaidi shauri namba 3 la Mwaka 2023, ambapo  Shahidi wa saba ametoa ushahidi wake.

Washitakiwa katika shauri hilo kwa pamoja wanakabiliwana kesi ya kula njama ya kutenda vitendo vya kigaidi kinyume na sheria ya kuzuia ugaidi namba 21 ya Mwaka 2002, ikisomwa pamoja na aya ya 24 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57 kifungu kidogo cha kwanza na kifungu cha 60 kifungu kidogo cha pili cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 ya Mwaka 2023

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Salmu Haruna,Hussein Juma,Fadhir Suleiman,Rashid Mussa,Hamis Daud,Amasha Abdallah,Nurdin Ibrahim, na Abdul Omari  wote ni wakazi wa kahama Mkoani Shinyanga,ambao walikamatwa katika tarehe na maeneo tofauti wilayani humo

Upande wa Jamhuri unawakilishwa na Wakili wa serikali mwandamizi Jenethreza kitaly, wakili wa serikali mwandamizi Careny Mrango, wakili wa serikali Juma Mahona na wakili wa serikali Shani Wampumbulya,

Mawakili wasomi wanaowatetea washtakiwa hao ni pamoja na wakili Geofrey Tuli,wakili Shaban Mvungi,wakili Elizabeth Luhigo,wakilim Phares Malengo,wakili Audax Costantine,wakili Getruda Faustine,wakili Chrisantus Chengula na wakili Frank Samwel

Jaji anayesikiliza kesi hiyo ni mheshimiwa Geofrey Isaya

Washtakiwa.Jopo la Mawakili wasomi upande wa utetezi.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post