KLABU YA MAADILI YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA SERIKALI YAZIELEKEZA SHULE NA VYUO KUANZISHA KLABU ZA MAADILI KWA WANAFUNZI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imezielekeza  shule na vyuo Mkoani hapa kuanzisha klabu za maadili kwa wanafunzi ili kuendelea kulinda na kuimarisha uadilifu kwa wanafunzi na jamii.

Maelekezo hayo yametolewa leo Jumatatu Oktoba 23,2023 na  kaimu katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Makana akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa klabu ya maadili Mkoa wa Shinyanga.

Amesema ni muhimu shule na vyuo Mkoani Shinyanga kuwa na klabu za maadili ili wanafunzi waweze kujifunza misingi  yenye maadili bora itakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku.

“Kutokana na umuhimu wa klabu hii katika kukuza maadili ya watanzania nazielekeza shule na vyuo vyote Mkoani Shinyanga kuanzisha klabu za maadili za wanafunzi na wanachuo ili kuwe na wanafunzi waadilifu”.

“Aidha mratibu wa maadili Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kufanya ufuatiliaji wa klabu hizo ngazi zote za shule na vyuo ili kuona zinafanyakazi kama ilivyokusudiwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuwa kunauhusiano mkubwa kati ya wanafunzi wenye maadili mema na kuongeza ufaulu katika masomo yao”.amesema Makana

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi (Simiyu, Shinyanga na Tabora) Bwana Gerald Mwaitebele amewasisitiza walimu kuwa na utaratibu wa wanafunzi wa klabu za maadili kutoa elimu ya maadili kwenye vikao vya wazazi shuleni.

“Kuna wazazi wengine ni changamoto kwa sababu ya kukosa uelewa lakini mnavikao vya wazazi shuleni sasa kabla ya kikao hakijaendelea wale watoto wanakuwa wameandaa ujumbe kupitia kwenye shairi au ngonjela kwahiyo katika vikao vya wazazi hakikisha klabu ya maadili inatoa elimu na wazazi wanapata maana wengine wanafanya kwakutokujua kwahiyo ni muhimu wapate elimu waweze kubadilika”.amesema Mwaitembele

Kwa upande wake afisa maadili kanda ya magharibi Onesmo Msalangu amesema klabu ya maadili ni kikundi au vikundi vya wanafunzi ndani ya shule au vyuo vyenye jukumu la kuratibu na kufanikisha shughuli za kuelimisha, kuhamasisha na kushirikisha jamii masuala ya maadili kwa ujumla.

Amesema lengo la klabu ya maadili nikuwajengea wanafunzi na wanavyuo misingi bora ya maadili tangu wakiwa shule na vyuoni ili kutengeneza Taifa la vijana waadilifu.

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo amesema  mambo yenye kudumisha uzalengo ni pamoja na kudumisha amani, kuipenda na kuiheshimu jamii, kuwa mwadilifu, kuwajibika, kujipenda na kuwapenda wengine, kudumisha demokrasia, kulinda rasilimali zetu, kutunza mazingira, kutii sheria, kuzingatia haki za binadamu zenye kujenga maadili pamoja na kuchukia kutoa au kupokea rushwa.

Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo wamewashukuru wawezeshaji wa elimu hiyo huku wakiahidi kwenda kutekeleza miongozi ya klabu ya maadili ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali.

Klabu ya maadili leo imezinduliwa rasmi Mkoa wa Shinyanga ambapo viongozi wametembelea  na kukagua klabu za maadili kwa wanafunzi katika shule ya sekondari Uhuru pamoja na shule ya msingi Town zilizopo Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Ibrahim  Makana akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele  akizungumza kwenye  mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele  akizungumza kwenye  mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akitoa mada ya uzalendo kwenye  mafunzo hayo ya klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Afisa maadili kanda ya magharibi Onesmo Msalangu akitoa mada ya mwongozo wa klabu za maadili kwenye  mafunzo hayo Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Walimu wa walezi wa klabu za maadili shule za msingi, sekondari na vyuo katika Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika mafunzo hay oleo Jumatatu Oktoba 23,2023

Walimu wa walezi wa klabu za maadili shule za msingi, sekondari na vyuo Manispaa ya  Shinyanga wakipongeza na kushukuru kwa hatua zilizofikiwa na klabu ya maadili.

Viongozi pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Walimu wa walezi wa klabu za maadili shule za msingi, sekondari na vyuo Manispaa ya  Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Viongozi wa klabu ya maadili wakitazama igizo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru baada ya kuwatembelea kwa lengo la kukagua klabu ya maadili kwa wanafunzi katika shule hiyo leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Uhuru 

Mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bakari Kasinyo akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru leo Jumatatu Oktoba 23,2023.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru leo Jumatatu Oktoba 23,2023

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi Gerald Mwaitebele akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari Uhuru leo Jumatatu Oktoba 23,2023

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post