MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MHE. MNDEME ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA TARAFA, WATENDAJI WA KATA, MITAA NA VIJIJI

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaagiza maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kusimamia matumizi ya fedha za Miradi ya maendeleo  ambazo zinatolewa na serikali katika maeneo yao.

Ametoa maagizo hayo leo wakati akizungumza na maafisa tarafa, watendaji wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

RC Mndeme amewataka viongozi hao kwenda kutekeleza maelekezo ya Rais  Dkt.Samia Saluhu Hassan kwa vitendo, katika sekta zote ambazo Serikali inatoa fedha kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu na miundombinu.

“Nendeni mkatafadhiri kwa vitendo maono ya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhaminia kuwaletea maendeleo watanzania sisi watendaji tunaowajibu wa kusimamia shughuli za maendeleo zote katika maeneo yetu nendeni mkatafadhiri maono ya Mhe. Rais kwa vitendo katika sekta zote sekta ya maji, sekta ya viwanda, sekta ya barabara, sekta ya afya , sekta ya elimu na sekta zingine zote bila uoga kasimamieni maono ya Mhe. Rais kwa ujasili ilimradi usivunje sheria”.

“Nendeni mkasimamie utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yenu fedha zinaziletwa na Mhe. Rais zisimamiwe kikamilifu pawepo na matumizi sahihi ya miradi lakini pia miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora, kasimamieni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi wa vitendo”.amesema RC Mndeme

“Nendeni mkasimamie na kupinga kwa vitendo ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua stahiki kwa wale wote ambao wanafanya ukatili kwenye jamii iwe ni ukatili wa watoto iweni ni ukatili wa wanawake na wanaume nendeni mkasimamie na kupinga ukatili huo likiwemo suala la ndoa za utotoni sasa tukisikia ndoa ya mwanafunzi imefungwa mtendaji wa eneo utajieleza ulikuwa wapi niwaombe sana wakurugenzi lisimamieni hili kuweni karibu na jamii zuieni vitendo vya ubakaji na ulawiti”.amesema RC Mndeme

“Simamieni ukusanyaji wa mapato hakikisheni hakuna mianya yoyote ya kuvuja kwa mapato ya Halmashauri na vilevile ongezeni vyanzo vya mapato katika maeneo yenu waambieni wananchi fedha zilizopokelewa za miradi katika maeneo yetu suala lingine ni ulinzi na usalama hakikisheni kila mmoja eneo lake linakuwa salama kuweni na orodha ya wakazi katika maeneo yetu jiepushenui kupokea watu msiowafahamu likiwemo suala la wahamiaji haramu mkalisimamie”.

“Ninyi watendaji mnawajibu wa kutatua kero za wananchi katika maeneo yetu msisubiri mpaka viongozi wa juu nitahitaji kupata taarifa za utatuzi wa kero za wananchi za kila mwezi wasilisheni kwa makatibu tawala wa Wilaya, fungueni milango wazi lakini pia punguzeni kuchati na simu au kuongea na simu wakati wa kumhudumia wananchi nendeni mkawahudumie wananchi bila ubaguzi”.amesema RC Mndeme

“Nendeni mkasimamie na kuzuia utoro shuleni wale watoto wote walioacha shule nendeni mkawarudishe darasani ni haki yake motto kupata elimu, lakini pia nendeni mkatatue migogoro ya ardhi na mhakikishe mnazuia migogoro ya ardhi kwenye maeneo yenu pia mkazuie migogoro ya wakulima na wafugaji  tuishi kwa utii wa sheria”.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezungumzia uwepo wa mvua nyingi za wastani katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaagiza watendaji hao kutoa taarifa za tahadhari ya mvua kwa wananchi.

“Nendeni mkawaambie wananchi wachukue tahadhari ya mvua kwa kuwashirikisha maafisa ugani walime mazao ambayo yatafaa kwenye mvua hizi nyingi nendeni mkawaambie wananchi walioko kwenye maeneo hatarishi wachukue tahadhari na kuondoka kwenye maeneo hayolakini pia kasimamieni utunzaji wa mazingira pamoja na kuzingatia suala la usafi wa kila Jumamos ya mwisho wa mwezi”. Amesema RC Mndeme

 Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Samizi amewasisitiza viongozi hao kushirikiana na wananchi hasa katika hatua za utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika maeneo yao.

Nao baadhi wa watendaji wa kata, mitaa na vijiji wameahidi kutekeleza maagizo hayo kwa kufuata taratibu za Nchi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga, leo ameshiriki katika kikao cha pamoja na Maafisa tarafa, watendaji wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri tatu za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga vijijini.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Savana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa maagizo kwa maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akitoa maagizo kwa maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye kikao hicho leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu wa Uhamiaji Lydia Angumbwike akiomba ushirikiano kwenye kikao hicho leo Jumanne Oktoba 10,2023.

Kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na  maafisa Tarafa, Watendaji  wa kata, Mitaa na vijiji kutoka katika Halmashauri za Kishapu, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kikiendelea leo Jumanne Oktoba 10,2023 katika ukumbi wa Savana.











This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post