SKAUTI WILAYA YA SHINYANGA WAADHIMISHA NYERERE DAY, MADAM VERONICA AWASIHI WANANCHI KUENDELEZA UMOJA NA USHIRIKIANO.


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Naibu kamishna wa Skauti katika Wilaya ya Shinyanga Veronica Marwa amewasihi wakazi wa wilaya ya Shinyanga kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuendeleza hali ya umoja, ushirikiano na amani.

Ameyasema hayo  Jumamosi Oktoba 14 wakati vijana wa Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiadhimisha kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Nyerere, ambapo vijana hao wameadhimisha kumbukizi hiyo kwa kufanya matembezi ya amani na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi wa mazingira na upandaji wa miti.

Naibu Kamishina huyo amesema kupitia matembezi hayo ya amani yamelenga kuhamasisha wananchi juu ya upandaji wa miti pamoja na usafi wa mazingira huku akiwaomba wakazi wa Wilaya ya Shinyanga kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua uchumi wa Taifa.

“Katika kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira tumepanda miti zaidi ya mia moja lakini baadhi ya miche tumewagawia wananchi ili nao washiriki katika tukio la leo, nawaomba tuendeleze umoja wetu na mshikamano lakini pia usawa wa kijinsia tufanye kazi tuendelee kumuunga mkono Rais wetu wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazozifanya katika kukuza uchumi wa Nchi yetu lakini pia uchumi wa mtu mmoja mmoja”.amesema Madam Veronica

Kwa upande wake Afisa mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga amesema ni muhimu kutunza mazingira ili kuepukana na athari mbalimbali huku akiwasisitiza wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kuchukua tahadhari za uwepo wa mvua za El nino.

Mtendaji wa Kata ya Mjini Bwana Simon Mashishanga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga amewapongeza vijana wa skauti kwa kuadhimisha siku hiyo.

Vijana wa Skauti Wilaya ya Shinyanga leo Jumamosi Oktoba 14,2023 wamefanya matembezi ya amani yaliyolenga kuhamasisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo yamefanyika Jumamos Oktoba 14,2023 katika Manispaa ya Shinyanga.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo yamefanyika  Jumamos Oktoba 14,2023 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga.

Skauti Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika matembezi ya amani ya kumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo yamefanyika  Jumamos Oktoba 14,2023 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post