SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YATOA ELIMU YA UKATILI TINDE GIRLS HIGH SCHOOL WANAFUNZI WAIPONGEZA

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi amewasihi wanafunzi wa Tinde Girls High school kusoma kwa bidii na kuacha tamaa zinazopelekea athari mbalimbali ikiwemo ukatili.

Ameyasema hayo  Jumatano Oktoba 18,2023 wakati viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wakitoa elimu ya ukatili katika shule hiyo ya Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Bi.Nabila Kisendi amewasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waweze kufikia malengo yao huku akiwasisitiza kuepuka tamaa ikiwa ni pamoja na kujiepusha na mahusiano ya kimapenzi wakati bado wanasoma.

Amesema athari za kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi wakati bado wanafunzi ni  mimba na ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na athari za magonjwa mbalimbali hali ambayo inatajwa kukwamisha ndoto nyingi za wanafunzi wa kike.

Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti Kisendi amewasisitiza wanafunzi hao kuwa na uthubutu ambapo amewaomba kutofumbia macha ukatili wowote wanaokutana nao  na kwamba wanapaswa kutoa taarifa sehemu husika ili hatua zaidi ya kisheria ziweze kuchukuliwa na serikali.

Viongozi wengine akiwemo katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapata, Mwenyekiti idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Nalinga (Cheupe), Mwenyekiti idara ya Michezo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga afande Willa Alkwin, Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Stella Gershom  pamoja na katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Hasna Maige wametoa elimu ya ukatili katika shule hiyo ya Tinde Girls High school.

Viongozi hao wamezungumzia athari za aina mbalimbali za ukatili ikiwemo ukatili wa kijinsia, ukatili wa kisaikloji na ukatili wa kingono huku wakiwasihi wanafunzi hao kuepukana na vitendo vya  ukatili kwa kuhakikisha wanatoa taarifa za ukatili unaofanyika hasa shuleni, kutoa taarifa kwa walimu au kupiga simu namba ya bure 116.

Baadhi ya wanafunzi wa Tinde Girls school wamewapongeza viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa elimu hiyo ambapo wamesema itawasaidia kujilinda ili waweze kufikia malengo yao huku wakiahidi kuwa mabalozi wazuri wa kupambana na ukatili unaoendelea kufanyika.

SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili inayotekeleza majukumu yake chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum ambapo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imeendelea kutoa elimu ya ukatili katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA Mkoa na Wilaya ya Shinyanga vijijini wakiwasili shuleni kwa ajili ya kutoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school.

Mwenyekiti wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Katibu wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akitoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa idara ya maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe)  akitoa elimu ya ukatili unaosababishwa na mmomonyoko wa maadili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa idara ya Michezo SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Polisi wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga, afande Alkwin Willa  akizungumzia umuhimu wa Michezo  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa SMAUJATA kanda ya Kahama Dr.Tamba akitoa elimu ya ukatili  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Stella Gershom  akitoa elimu ya ukatili  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Stella Gershom  akitoa elimu ya ukatili  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Katibu wa SMAUJATA Manispaa ya Shinyanga Hasna Maige akitoa elimu ya ukatili  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Shinyanga vijijini Bwana Emmanuel Makolo  akitoa elimu ya ukatili  kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Burudani ikiendelea.

Hafla ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kutoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school ikiendelea katika ukumbi wa mikutano wa shule hiyo.

Hafla ya SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kutoa elimu ya ukatili kwa wanafunzi wa Tinde Girls High school ikiendelea katika ukumbi wa mikutano wa shule hiyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post