WANAFUNZI SHINYANGA WATAKIWA KUWEKA BIDII, JUHUDI NA MAARIFA KWENYE MASOMO YAO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele, amewataka  wanafunzi kuweka bidii,juhudi na maarifa kwenye masomo, kama hatua ya kukabiliana na ushindani katika soko la Elimu na  ajira

Akizungumza na wanafunzi wa klabu ya maadili katika shule ya Sekondari Uhuru na Town  Shule ya Msingi zilizopo katika Manispaa  ya Shinyanga, ambapo amewataka kuepuka tama na vishawishi.

Mwaitebele amewasisitiza wanafunzi hao kujitunza na kujilinda dhidi ya mazingira hatarishi yanayoweza kuwasababishia kufanyiwa ukatili wa kijinsia

Kwa upande wake  mratibu wa klabu za maadili Mkoa wa Shinyanga Bwana Bakari Kasinyo amewataka wanafunzi hao kuzingatia uadilifu ili waweze kuhitimu masomo yao salama.

Baadhi ya wanafunzi wa klabu ya maadili katika shule za sekondari Uhuru  na Town shule ya msingi wameahidi kusoma kwa bidii huku wakieleza umuhimu wa klabu ya maadili shuleni.

Viongozi wa klabu ya maadili kanda ya magharibi na viongozi wa klabu ya Mkoa wa Shinyanga wametembelea baadhi ya Shule zenye klabu ya maadili katika Manispaa ya Shinyanga ikiwemo Shule ya sekondari Uhuru, shule ya msingi Town pamoja na shule ya Msingi Jomu.

Katibu msaidizi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi Gerald Mwaitebele akizungumza.Wanafunzi shule ya sekondari Uhuru.

Picha ya pamoja katika shule ya msingi Town

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post