KUELEKEA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MWENYEKITI WA SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA BI. NABILA KISENDI ATOA MAELEKEZO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Kuelekea kwenye kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi amewataka viongozi wa SMAUJATA Halmashauri zote sita za Mkoa wa Shinyanga kwenda kutoa elimu kwa wananchi.

Ameyasema hayo kwenye kikao cha pamoja cha viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga kilichojumuisha wenyeviti na makatibu kutoka kwenye Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti Kisendi amewasisitiza viongozi hao kwenda kushirikiana na viongozi wa serikali katika kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu ya ukatili kupitia vyombo vya habari pamoja na mikutano ya hadhara.

“Twende tukashirikiane na viongozi wa serikali waliopo kwenye Wilaya zetu ili kuweza kufikia malengo ya kiserikali niwaombe kwa yale ambayo tumeyazungumzia leo tukayafanyie kazi tunajukumu kubwa sana la kupinga na kutokomeza ukatili ndani ya Mkoa wetu wa Shinyanga”.

“Tupo ndani ya siku 16 zinazoanza tarehe 25 Novemba mpaka tarehe 10 Disemba hizi ni siku maalum za kupinga ukatili wa kijinsia kwahiyo tunanafasi kubwa sana tulipo kwenye maeneo yetu kuna Redio mliopo Shinyanga mnaweza kufika Redio Faraja kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya kupinga ukatili wa kijinsia pia tunaweza kuitisha hata vikao vya nzengo au mikutano ya hadhara lengo ni kufikisha ujumbe kule kwa wananchi tuwaombe viongozi wa serikali wanapokuwa na mikutano ya hadhara watushirikishe ndani ya siku hizi 16 tuwe tumetoa elimua ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yetu”.amesema Madam Kisendi

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya amewataka viongozi hao kuwa wazalendo katika kupambana na vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kuwajibika kwa kuhakikisha kila kiongozi anatimiza wajibu wake kupitia nafasi aliyonayo.

Mwenyekiti wa maadili SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Najulwa (Cheupe) amewasisitiza viongozi kuwa wanyenyekevu na kutumia lugha nzuri ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya staha ili kuwa watu wa mfano katika jamii wanaoishi.

Kwa upande wake Bi. Sophia Kang’ombe ambaye pia ni afisa ustawi wa jamii na msimamizi wa kituo cha wazee na wasiojiweza Kolandoto Mkoa wa Shinyanga amekemea mmomonyoko wa maadili unaosababisha ukatili katika jamii huku akiitaka jamii kupaza sauti kuhusu ukatili na madhara yanayojitokeza ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa na serikali.

Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini inayotekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Kampeni hiyo ambayo ilianzishwa na Mwenyekiti wa SMAUJATA Taifa shujaa Sospeter Bulugu kwa kushirikiana na Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima.Aidha katika kikao hicho pamoja na mambo mengine wamezungumzia ujio wa katibu wa SMAUJATA kanda ya Ziwa ambaye anatarajia kufanya ziara yake mwanzoni wa Mwezi ujao wa Disemba 2023.Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa kampeni hiyo wakiwemo wenyeviti na katibu kutoka kwenye kila Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bi. Nabila Kisendi akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa kampeni hiyo wakiwemo wenyeviti na katibu kutoka kwenye kila Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.Wenyeviti na katibu wa SMAUJATA kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha pamoja.





This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post