MBUNGE MHE. KATAMBI AIPONGEZA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI KWA UBUNIFU, MRADI WA UFYATUAJI TOFALI KUANZA KUTUMIKA MWEZI UJAO

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi ameipongeza jumuiya ya umoja wa wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kuanzisha mradi wa ufyatuaji tofali utakao wanufaisha na kutoa fursa mbalimbali kwa wananchi.

Ametoa pongezi hizo leo Jumamos Disemba 16,2023 wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini, baada ya kutembelea mradi huo wa ufyatuaji tofari ulioanzishwa na jumuiya hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi wao na kutoa fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Katambi ameipongeza jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kwa ubunifu wao ambapo amewasihi kuwa waaminifu katika utekelezaji wa mradi huo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na jumuiya hiyo katika utatuzi wa changamoto zilizopo ili kufikia malengo waliyojiwekea.

“Nimefika kwenye eneo la mradi kwa kweli nimefurahishwa sana kwanza niwapongeza sana viongozi wa jumuiya hii kwa kuwa wabunifu na hiki ndicho kinachotakiwa na serikali yetu lakini zaidi chama chetu cha mapinduzi hii ni sehemu ya kusaidia serikali kwenye suala la ajira lakini pia kuchangia kwenye pato la Taifa kwa maana ya kujenga uchumi niwaombe tu mradi huu uwe endelevu na uzalishe ajira na tutafute masoko kwa kujinadi kupitia bidhaa tunayoizarisha na mimi nitaendelea kushirikiana nanyi katika kuendeleza mradi huu”amesema Mhe. Katambi.

Katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Yotham Kibabi wakati akisoma taarifa fupi amesema mradi wa ufyatuaji tofali aina ya Block unatarajiwa kuanza kutumia rasmi  mwezi Januari Mwaka 2024.

Mradi huo upo katika Manispaa ya Shinyanga karibu na kituo cha afya Kambarage ambapo pamoja na mambo mengine jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini imetoa vyeti vya pongezi na kuvishukuru ofisi, viongozi na wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha mradi wa ufyatuaji tofari ikiwemo ofisi ya jumuiya ya wazazi Taifa pamoja na mjumbe wa Halmashauri kuu wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana James Jumbe.

“Hali ya mradi mpaka sasa tumeshanunua mashine mbili za ufyatuaji tofari ambapo mashine moja niyakutumia mkono mashine nyingine niyakutumia umeme lakini pia tumejenga banda la kuwekea mashine , tumevuta maji umeme fezi three umeme wa kiwandani, tumeshavuta bomba la maji, tumejenga sink la maji, tumeshachonga vibao vya kufyatua tofari pamoja na mapipa ya maji yatakayotumika sehemu ya kazi za nje”.

“Tunaishukuru ofisi ya umoja wa wazazi CCM Taifa chini ya Bwana Gilbert Kalima ambaye ni katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi Taifa (MNEC) kwa kutusaidia kiasi cha fedha za kuendeleza mradi, pili tunaishukuru ofisi ya CCM Mkoa wa Shinyanga kwa kutupatia eneo la kuanzishia mradi wetu, tatu tunawashukuru wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya ya Shinyanga kupitia kwa katibu wa CCM Wilaya tunawashukuru kwa kutupatia fedha za ununuzi wa mashine ya kukatia risiti EFD, nne tunawashukuru wote waliotuchangia michango ya kufanikisha mradi”.

“Shukurani za kipekee zimwendee Ndugu James Jumbe Wiswa ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga na mjumbe wa kamati ya siasa Wilaya ya Shinyanga tunamshukuru kwa kununua mashine mbili za kufyatua tofari aina ya Block na kutoa fedha za uvutaji wa umeme pamoja na kusaidia shughuli mbalimbali za jumuiya ya wazazi katika kujiimarisha kisiasa na kiuchumi”.amesema katibu Doris

Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko amesema kupitia mradi huo wa kufyatua tofali wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Shinyanga watapata ajira kwa kuzingatia uwezo wa mtu bila kuangatia chama cha siasa huku akiwaomba kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa zitakazopatikana kwenye mradi huo.

Naye Mjumbe wa kamati ya siasa, mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM Wilaya na Mkoa wa Shinyanga, mjumbe wa baraza kuu Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa mkutano mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa ameahidi kuendelea kutatua changamoto kadri ya uwezo wake kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuchochea uchumi Nchini.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Paschal Patrobas Katambi akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamos Disemba 16,2023.

Katibu wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Doris Kibabi akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamos Disemba 16,2023.

Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamos Disemba 16,2023.

 Mjumbe wa kamati ya siasa, mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM Wilaya na Mkoa wa Shinyanga, mjumbe wa baraza kuu Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa mkutano mkuu Mkoa wa Shinyanga Mhandisi James Jumbe Wiswa akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamos Disemba 16,2023.

 

Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Peter Frank Alex ( Mr. Black) akizungumza kwenye kikao cha baraza la jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Jumamos Disemba 16,2023.






This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post