MWENYEKITI MTAA WA DOME BWANA NAJULWA (CHEUPE) AFUNGA MWAKA NA MKUTANO WA HADHARA SHINYANGA

Serikali ya mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi imeendelea kutokumeza vitendo mbalimbali vya uhalifu ikiwemo wizi na vitendo vya ukatili na kwamba hatua hiyo imesaidia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa leo Disemba 31,2023 kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi kuanzia Mwezi Oktoba hadi mwezi Disemba Mwaka 2023.

Mwenyekiti huyo amesema ameendelea kushirikiana na jeshi la polisi akiwemo polisi kata wa kata ya Ndembezi kwa kushirikiana na wananchi kuzuia uhalifu ambapo pamoja na mambo mengine amesema serikali ya mtaa huo imefanikiwa kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya kifamilia 26.

“Tumeweza kusuluhisha migogoro mbalimbali ya kifamilia ipatayo 26 mpaka sasa zinaendelea vizuri, lakini pia katika kipindi hicho tumeweza kuwaandikia watu 70 barua za utambulisho wanaoenda maeneo mengine, kuhusu suala la ajira tumewasainia vijana wa kike na wakiume 22 kupata kazi sehemu mbalimbali, tumewasainia barua za mikopo jumla ya wakazi 238 wanaume kwa wanawake sehemu mbalimbali za mashirika kifedha”.

“Katika suala la miundombinu serikali imeweza kuleta miradi ya barabara katika mtaa wetu wa Dome jumla ya kilomenta 1.8 zimetengenezwa na wakala wa barabara TARURA kwa kiwango cha molamu lakini pia kwenye suala la huduma ya afya jumla ya wazee 13 tumewaandikia barua za msamaha wa matibabu kwenye Hospitali yetu ya Mkoa katika suala la mazingira tumeendelea kutunza bustani kwa kushirikiana na walengwa wa tasaf tukishirikiana na mzabuni Joseph Kisango katika mradi wa Dome”. amesema Mwenyekiti Najulwa

“Suala la ulinzi na usalama tumeendelea kushirikiana na jeshi letu la Polisi chini ya kamanda Janeth Magomi tumekuwa naye kwa kusaidizana na kijana wake polisi kata wetu ni askari ambaye ukimpigia simu yuko vizuri usiku na mchana lakini pia tumeendelea kutokomeza vitendo vyote vya uovu kwa kushirikiana na wananchi ambapo wanatoa taarifa za viashilikia vya uhalifu mpaka sasa usalama kwenye mtaa huu ni shwari”.amesema Mwenyekiti Najulwa

Polisi jamii wa kata ya Ndembezi Jastin Nyatano amewataka wananchi kutojihusisha na uhalifu huku akiwakumbusha  kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu utakaojitokeza hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Mwaka mpya ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Katika mkutano huo wa hadhara afisa habari wa jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Shinyanga Helen Amour ametoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhara ili kuepukana na majanga hao.

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Dome waliohudhuria mkutano huo wamepongeza kwa juhudi zinazofanywa na serikali hiyo huku wakishukuru kwa kupata elimu ya kukabiliana na majanga ya moto.


Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Bwana Solomon Nalinga Najulwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa kazi kuanzia Mwezi Oktoba hadi mwezi Disemba Mwaka 2023.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post