SHUWASA YAWATOA HOFU WATEJA WAKE HUDUMA YA MAJI KUREJEA MUDA WOWOTE MJINI SHINYANGA

Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard (Manka) akizungumzia changamoto ya kukatika kwa huduma ya maji.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamesema hali ya kukatika kwa maji mara kwa mara imekuwa ikisababisha usumbufu kwa watumiaji wa huduma hiyo majumbani na kwenye maeneo ya Biashara.

Wamelalamikia hali hiyo wakidai kuwa ni usumbufu na kwamba imekuwa ikisababisha hatari katika uendeshaji wa shughuli za kibiashara ambazo zinategemea huduma ya maji.

Wameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Shinyanga SHUWASA kutoa ratiba ya uhakika ili kuwawezesha watumiaji kuhifadhi maji ya kutosha,kuliko hivi sasa ambapo taarifa zinazotolewa zinakuwa hazieleweki.

Kutokana na malalamiko hayo Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard ambaye ametoa ufafanuzi juu ya changamoto hiyo.

“Tulikuwa na changamoto ya huduma ya maji kwa Manispaa ya Shinyanga pamoja na miji midogo ya Tinde, Didia na Iselamagazi  changamoto hiyo ilianza tarehe nne mpaka tarehe nane lakini ilitokana na wenzetu wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira KASHUWASA  walikuwa wameacha uzalishaji wa mitando yao ya maji katika mitambo yao ya maji  iliyopo Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza kutokana na majaribio ya mfumo mpya ya kuweka dawa zoezi hilo lilichukua takribani siku tatu baada ya hapo huduma ilirejea kama kawaida”.amesema Nsianeli

“Tarehe tisa tulipata tena changamoto katika mradi huo wa uzalishaji maji wa KASHUWASA ambapo nguzo za umeme zilianguka na wataalam wa TANESCO walikuwa wanaendelea na marekebisho lakini hadi kufikia leo asubuhi huduma ilikuwa bado haijarejea, lakini muda huu tumefanya mawasiliano na watu wa tenki la Old Shinyanga wamesema maji yameanza kuongia ingawa yanamgandamizo kidogo”.

“Tukirudi kwa upande wetu SHUWASA tuna bwawa la Nhimwa kwa tarehe 4 mpaka 8 tulikuwa na changamoto ya mifumo ya mashine zilizopo pale lakini juhudi zilifanyika mpaka tarehe 8 asubuhu tuliweza kuzalisha maji yetu ya Nhimwa lakini isipokuwa jana usiku umeme katika maeneo ya mitambo ya Nhimwa hakuna kwahiyo uzalishaji umesimama mpaka sasa”.amesema Nsianeli

Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard (Manka) amewatoa hofu wateja wake huku akieleza kuwa juhudi mbalimbali za kurejesha huduma zinaendelea.

Akizungumzia changamoto hiyo  mhandisi wa mipango kutoka shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Shinyanga Hassan Koko amesema changamoto hiyo inatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.

“Kweli tunachangamoto ya umeme maeneo ya kuanzia Nhimwa kuelekea Mwakitolyo mpaka Iselemagazi Old Shinyanga na hii changamoto imetokana na nguzo yetu moja kubwa ya laini kubwa ilipata hitilafu jana usiku saa tisa kwa kukatika upande wa juu mpaka sasa mafundi wapo saiti wanaendelea na kazi matumaini yetu ifikapo jioni kazi itakuwa imekamilika na wateja wetu watapata huduma ya umeme”.amesema Mhandisi Koko

 Afisa mahusiano na mawasiliano SHUWASA Bi. Nsianeli Gelard (Manka) akizungumzia changamoto ya kukatika kwa huduma ya maji.

Mhandisi wa mipango kutoka shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Shinyanga Hassan Koko akititolea ufafanuzi changamoto hiyo.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post