SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA YAKEMEA NA KULAANI VIKALI UKATILI WA WA KIJINSIA, WANAFUNZI WAELEZA KUNYIMWA HAKI YAO YA ELIMU.

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imekemea na kulaani vikali ukatili wa kijinsia unaoendelea kwenye jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu huku ikiahidi kuendelea kutetea haki za watoto ikiwemo kutoa elimu ili waweze kutimiza malengo yao.

Hayo yamebainishwa na katibu wa kampeni ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya pamoja na katibu wa SMAUJATA Wilaya ya Kishapu Bwana James Onyango Daniel ambapo wamesema ni vyema jamii kuendelea kutoa taarifa za ukatili ili ziweze kushughulikiwa.

Viongozi hao wamekemea na kulaani vikali ukatili unaoendelea kufanyika kwenye baadhi ya familia mbapo baadhi ya wazazi ama walezi huwazuia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kuhitimu ikiwa lengo lao wasifaulu watoto wa kike waolewe.

SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imeahidi kuendelea kuibua masuala ya ukatili wa kijinsia hasa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Awali wakizungumza baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu  wameeleza  kuwa suala la watoto wa kike  wanafunzi kukosa haki yao ya elimu bado linafanywa na baadhi ya wazazi katika shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Wanafunzi hao wamesema baadhi ya wazazi wamekuwa kikwazo kwenye elimu ya watoto wao,wakitaka kuwaozesha ili wapate mali (Ng’ombe) wakiamini kuwa mali hizo ndiyo nguvu yao ya malezi.

Wamesema moja ya changamoto wanayokutana nayo wanafunzi wa kike ni kunyimwa mahitaji yao ya msingi ambapo wameiomba serikali na wadau kuendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wazazi na walezi katika Halmashauri hiyo.

Baadhi ya wazazi wa Wilaya ya Kishapu wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo huku wakiomba serikali na wadau kuendelea kutoa elimu na kwamba changamoto ya wanafunzi wa kike kupata mimba bado inaendelea katika shule za msingi na sekondari.

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amewataka wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla Wilaya ya Kishapu kushirikiana katika kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa taarifa za wahalifu kwa wakati ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.TAZAMA PICHA VIONGOZI WA SMAUJATA WAKISHIRIKI KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI YA ONGEA NAO KATIKA WILAYA YA KISHAPU.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post