WAZIRI MHE. SILAA AWASILI SHINYANGA NA KUTOA SIKU SABA KWA KATIBU MKUU WA WIRAZA HIYO PAMOJA NA MSAJILI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA


Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Jerry Silaa ametoa siku saba kwa katibu mkuu wa Wizara hiyo kushughulikia mgogoro wa ardhi baina ya halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Nyang’wale Mkoa wa Geita.

Ametoa agizo hilo leo Jumatatu Disemba 4,2023 wakati akizungumza na baadhi ya viongozi maafisa na watumishi wa idara ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga wakiwemo wakuu waWilaya na wabunge kutoka kwenye majimbo ya Mkoa wa Shinyanga.

Waziri Mhe. Silaa kufuatia hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje kuhusu mgogoro huo, ambapo amemwelekeza  katibu mkuu wa Wizara hiyo kuhakikisha timu inayoongozwa na wakurugenzi wa upimaji ramani wanafika na kushughulikia changamoto hiyo.

Katika agizo hilo pia Waziri Mhe. Silaa amemtaka msajili wa mabaraza ya ardhi na nyumba kufika Mkoani Shinyanga ndani ya siku saba na kwamba .

“Suala la mpaka baina ya Nyang’wale na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga naomba kusema mambo mawili la kwanza na namwelekeza katibu mkuu ndani ya siku saba kuansia leo ahakikishe timu  inayoongozwa na wakurugenzi wa upimaji na ramani ifike kwenye mpaka huo lakini  jambo la pili ndani ya siku saba hizo hizo msajili wa mabaraza ya ardhi na nyumba afike Shinyanga na taarifa zao nizipate kabla ya terehe 14 Mwezi huu wa kumi na mbili”.amesema Waziri Silaa

Aidha Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka watumishi wa ardhi kufanyakazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia taaluma zao.

Kwa upande wake kamishna msaidizi wa ardhi Mkoa wa Shinyanga Leo Komba amesema Mkoa wa Shinyanga umefanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na wizara huku akiahidi kuendelea kushughulikia changamoto zinazojitokeza.

Mkuu wa idara ya ardhi Wilaya ya Kahama Clemence Mkusa akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa idara hiyo ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wizara hiyo.

Waziri Mhe. Silaa amefika Mkoani Shinyanga kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi.

 

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Jerry Silaa akizungumza na baadhi ya viongozi maafisa na watumishi wa idara ya ardhi pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga wakiwemo wakuu waWilaya na wabunge kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya baraza la mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Mkuu wa idara ya ardhi Wilaya ya Kahama Clemence Mkusa akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine wa idara hiyo leo Jumatatu Disemba 4,2023 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post