MAKONDA AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUWAHUDUMIA KWA HAKI NA USAWA


Na Mapuli Kitina Misalaba

Katibu wa Siasa,uenezi na mafunzo  wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Mhe. Paul Makonda amewataka watumishi wa Serikali kuwahudumia Wananchi kwa haki na usawa  na kwamba watakaobainika kushindwa kuwahudumia wananchi hawatavumiliwa.

Ameyasema hayo leo Jumapili Januari 28,2024 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Town mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza viongozi kutimiza wajibu wao kwa wananchi wote bila kujali hali zao.

Mhe. Makonda ametahadharisha watumishi hao wa serikali wanaoshindwa kuwahudumia wananchi, kutetea na kulinda maslahi yao ambapo amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa kwa haki na usawa.

Pia ameonya kuhusu watumishi wanaotumia vyeo vyao kuminya haki za wananchi na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Yule anayeonea watu anayethurumu watu anayetumia cheto chake bila kujali utu huyo sitakuwa sehemu yake na kwa namna hii naomba niwaambie watumishi wa serikali wote wa ngazi zote, ukiharibu Chama hiki cha Mapinduzi msemaji wake ni Makonda siwezi kukutetea utabeba mzigo wako mwenyewe”.

“Kwahiyo kama kuna mtumishi amezoea kuwanyima haki wananchi kama kuna mtumishi hawathamini wananchi kama waajili wake CCM ya Samia haitambeba na msemaji wake ni Makonda nitafanya kwa mujibu wa sheria”.amesema Mhe. Makonda

Katibu huyo pamoja na mambo mengine amesikiliza na kutatua kero za wananchi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kwenye mkutano huo  ambapo wamemshukuru na kumpongeza kwa hatua hiyo ya kusikiliza changamoto zao.

Katibu wa Siasa,uenezi na mafunzo  wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Bwana Paul Makonda leo ametatua changamoto za wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mikoa mbali mbali Nchini ambapo jana alikuwa  Wilayani kahama na kwamba Mkoa wa Shinyanga ni Mkoa wa 9 katika ziara zake.

Aidha mkutano umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini, Vyama vya siasa, viongozi wa kimila pamoja na viongozi wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme, mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi Janeth Magomi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Paschal Patrobas Katambi, Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali.

 

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post