Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amekabidhi pikipiki 42 kwa jumuiya za watoa huduma za maji katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara ili kurahisisha utendaji kazi kwa watumiaji hao.
Pikipiki hizo zimetolewa na Wakala wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe. Sendiga amesema ni vyema kwa watumishi hao kuzitunza kwani ni mali ya serikali.
"Niwasihi tukahakikishe pikipiki hizi zinaenda kutumika kama ilivyokusudiwa na kuhakikisha skimu za maji zinakuwa endelevu na Wananchi wanapata huduma ya maji muda wote kwani ni haki yao ya msingi", amesema Mhe. Sendiga.
Aidha, Mhe. Sendiga amewataka wakuu wa taasisi mbali mbali kukusanya fedha za Umma kwa uadilifu kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo na kusitokee chombo chochote kukiuka kwa sababu yoyote huku akiwasihi wakuu wa wilaya wote kuendelea kusimamia vyema uhai wa miradi iliyojengwa.
"Serikali imewekeza fedha nyingi sana kujenga miradi hii ya maji, fedha hizi ni zenu kupitia kodi na tozo mbalimbali, tunajukumu kubwa la kuitunza miradi ili kuhakikisha kusudi la Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan la kumtua mama ndoo kichwani linafikiwa", amesema Mhe. Sendiga.
Akitoa shukrani zake kwa RUWASA Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange amesema kuwa atasimamia na kufuatilia kwa Ukaribu kama watumisji waliokabidhiwa pikipiki hizo wanazifanyi kazi kama ambavyo kusudio la Serikali ilivyowaagiza.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara Injinia Wolter Kilter amesema lengo la kuwapa pikipiki hizo kwa watumiaji hao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji kwa uharaha zaidi.
Amesema kuwa Mkoa wa Manyara unajumla ya Vyombo hivi 88 vinavyosimamia Skimu za maji 346 na kuhudumia wananchi 1,268,239 ambapo mpaka Septemba 30, 2023 zilikusanywa jumla ya Tshs 2,113,232,529", amesema Injinia Kilter.
Ameongeza kuwa RUWASA inaendelea kuvipatia mafunzo jumuiya za watumiaji Maji kama jinsi ya kuandaa mpango wa biashara na ufungaji wa hesabu, vyombo 32 vimeshapatiwa mafunzo hayo mpaka Julai 23, 2023.