Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika
la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) kwa ufadhili wa kifedha kutoka
shirika la Norwegian Church Aid (NCA); limeendesha mafunzo yakuongeza thamani
kwenye mazao hasa Nyanya, kwa wakulima pamoja na wadau wengine wa kilimo kutoka
kata za Sekebugolo na Mondo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa mikutano kijiji cha Mwigumbi Wilaya ya Kishapu na kwamba yameandaliwa na shirika la TCRS huku wawezeshaji wakitoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga.
Wakulima
20 walioshiriki mafunzo hayo wamepewa vyeti wakiwemo wafanyabiashara wa zao la
Nyanya kutoka kwenye vijiji vinne ambavyo ni Mipa, Dulisi, Weshiteleja pamoja
na kijiji cha Sekeididi na kwamba wamepewa mafunzo mbalimbali ikiwemo
usindikaji wa zao la nyanya ili kupata Tomato Sauce and Tomato
Paste.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo afisa uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa Shinyanga Joseph Taban amewasisitiza washiriki baada ya kupata elimu hiyo, kujiendeleza zaidi na ujuzi huo ili waweze kunufaika wao na jamii kwa ujumla.
“Baada
ya mafunzo haya na leo hii tumetunukiwa vyeti yasiishie hapa hapa ni lazima
tuhakikishe kwamba ujuzi huu tulioupata ukawe na manufaa kwetu na watu wengine
wanaotuzunguka, hapa umepata ujuzi lakini ili uweze kuwa na manufaa, ujuzi huu
ni wewe kuendelea kufanyia mazoezi hata kabla hujaanza kuanzisha hicho kiwanda
kidogo cha usindikaji anza kusindika kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani kwanza
halafu badaye utakavyokuwa unafanya mara kwa mara utakuwa unagundua na vitu
vingine ambavyo hukujifunza awali”.amesema Taban
Kwa
upande wake afisa uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka SIDO Bwana Abel
Bebwa amewasihi washiriki hao kujiamini zaidi kwenye utekelezaji wa majukumu
yao ikiwemo kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika Maisha ya kila siku.
Naye afisa Kilimo kutoka shirika la TCRS Wilaya ya Shinyanga Bwana Laurent Stanslaus amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo hasa kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao la Nyanya.
“Mafunzo
haya yanalenga hasa kuweza kupunguza matatizo ambayo yanatokana na uharibifu wa
chakula kwa sababu kuna muda wakulima wanavuna mazao mengi hasa mazao
yanayowahi kuharibika mfano zao la Nyanya akivuna halafu unakuta soko ni
changamoto kwahiyo tumeona kwamba tuwape mafunzo haya ili mkulima aweze kuwa na
uwezo wa kufaidika na mazao anayoyapata”.amesema Stanslaus
Washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru TCRS, NCA pamoja na shirika la SIDO kwa kuwapa elimu hiyo ambayo wamesema itawasaidia kuinuka kiuchumi hasa katika Biashara pamoja na shughuli zingine za kwenye familia zao ikiwemo kusomesha watoto.
Afisa
uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO
Bwana Abel Bebwa akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo hayo kuhusu mambo
muhimu ya kuzingatia katika usindikaji wa sosi ya Nyanya.
Washiriki wakiandaa mahitaji muhimu ikiwemo vitunguu maji, Chumvi, Sukari, Pilipili manga kwa ajili ya usindikaji wa sosi ya Nyanya.

Washiriki wakiandaa mahitaji muhimu ikiwemo Nyanya, vitunguu maji, Chumvi, Sukari, Pilipili manga kwa ajili ya usindikaji wa sosi ya Nyanya.
Afisa
uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO
Bwana Abel Bebwa (kulia) akikabidhi cheti kwa mshiriki ambaye amehitimu mafunzo
ya usindikaji vyakula (Tomato Sauce and Paste) yaliyoandaliwa na shirika la
TCRS Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Zoezi
la kukabidhi vyeti kwa washiriki kwa ajili ya mafunzo ya usindikaji vyakula (Tomato Sauce
and Paste) yaliyoandaliwa na shirika la TCRS Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
likiendelea.

uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa
Shinyanga Bwana Joseph Taban akiwasisitiza washiriki kuendeleza ujuzi
walioupata kwenye mafunzo hayo.
Afisa
uendeshaji Biashara kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO Mkoa wa
Shinyanga Bwana Joseph Taban akiwasisitiza washiriki kuendeleza ujuzi
walioupata kwenye mafunzo hayo.
Afisa
uendeshaji Biashara mwandamizi kutoka shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO
Bwana Abel Bebwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa
Kilimo kutoka shirika la TCRS Wilaya ya Shinyanga Bwana Laurent Stanslaus akizungumzia
umuhimu wa mafunzo hayo kwa wakulima na wafanyabiashara hasa wa zao la Nyanya.
Viongozi
na washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.