Na Mapuli Kitina Misalaba
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga (inajumuisha
Mikoa miwili Shinyanga na Simiyu) Frank Habibu Mahimbali amewataka wananchi kutumia
mfumo wa TEHAMA katika kufungua mashauri ili kuondoa malalamiko
yanayosababishwa na ucheleweshaji wa kesi
mahakamani.
Ametoa wito huo Alhamis Februari mos kwenye kilele cha
maadhimisho ya wiki na siku ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama
Kuu Kanda ya Shinyanga wakati
akizungumzia umuhimu wa mfumo jumuishi katika uendeshaji wa haki jinai ambapo
amewataka wananchi kuwa tayari kupenda kutumia TEHAMA ili kupata taarifa zao
kwa wakati juu ya hatua mbalimbali za mashauri.
Amesema Mahakama hiyo imeporesha mfumo wa TEHAMA ili
kuendelea kutekeleza kwa vitendo dira ya utoaji haki kwa wakati kwa watu wote
huku akisisitiza kutumia mfumo huo ili kuepukana na changamoto ndogo ndogo
zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya wananchi.
“Mifumo
hii iko wazi na inapitika kwa kila mwananchi na kila mdau, mfumo huu umesaidia
mambo yafuatayo usajili wa mashauri kwa njia ya mtandao madali popote na muda
wowote siyo lazima ufika hapa Mahakamani lakini pia imetuwezesha upangaji wa
mashauri kwa majaji na mahakimu kwa (Kidgitali) lakini uandishi wa hukumu na
mienendo ya mashauri moja kwa moja kwenye mfumo tofauti na ilivyokuwa awal,
vituo mbalimbali vya Mahakama kusomana na mifumo ya wadau muhimu wa Mahakama
kama vile NIDA”.
“Faida
nyingine ni kuweka nyaraka katika mfumo digit mfumo huu unasaidia Mahakama na
wadau kusahau atha za upotevu wa nyaraka unaochangia na ucheleweshaji wa
mashauri pia mfumo huu umesaidia sana mashahidi kuweza kusikilizwa popote alipo
pasipo kupata atha ya kusafiri kufika Mahakamani nah ii inaokoa sana gharama za
fedha muda na kurahisisha usikilizwaji wa mashauri, mfumo huu pia unawezesha
wadau wa Mahakama kupata nyaraka mbalimbali kama vile hukumu uamuzi na sheria
kwa njia ya elekronik ”.amesema Jaji mfadhi Frank
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Frank
Habibu Mahimbali ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji nzuri wa TEHAMA nchini huku
akimshukuru jaji Mkuu wa Tanzania profesa Ibrahim Juma kwa kuendelea kusimamia maboresha
ya haki jinai na matumizi ya TEHAMA kwenye Mahakama.
Mahimbali amewashukuru wananchi kwa ushiriki wao
katika maadhimisho ya wiki ya sheria huku akiwataka kutumia vyema elimu waliyoipata
katika maonyesho ya wiki ya sheria kwani ni chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika
jamii .
Amesema ni muhimu kutumia kutumia elimu hiyo ikiwemo
elimu ya masuala ya kisheria, kuleta mabadiliko chanya katika mtindo wa
maisha ya kila siku kisheria na kijamii.
Pamoja ma mambo mengine Jaji mahimbali amewataka
watumishi wa mahakama kanda ya Shinyanga kufanyakazi kwa kuzingatia misingi ya
sheria na kanuni zilizopo pamoja na kuwahudumia wananchi kwa weledi na
uadilifu.
Solomon Lwenge kutoka ofisi ya wakili mkuu wa serikali
kanda ya Shinyanga pamoja na mambo mengine amewasihi wadau wa haki jinai
kuendelea kushirikiana katika kutoa elimu kwa umma kuhusu uzingatiaji wa
utekelezaji wa sheria zinazohusu haki jinai kwa ustawi wa wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina
Mndeme amesema serikali itaendelea kushirikiana na muhimili wa Mahakama kwa
kuweka na kuboresha mazingira wezeshi na salama ili kurahisisha
upatikanaji wa haki kwa wakati.
Maadhimisho ya wiki ya sheria yalifunguliwa rasmi
Januari 24 ambapo kilele chake kimefikia hii leo February Mosi mwaka huu 2024
ambapo kaulimbiu ya Mwaka huu inasema “Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa
Taifa: nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi kwa haki
jinai”.
JAJI MFAWIDHI AKITAJA TAKWIMU ZA MASHAURI