RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI JUKWAA LA KODI NA UWEKEZAJI.

_Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akizungumza na vyombo vya habari (hawapo pichani), katika ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha_

Na Egidia Vedasto,

Arusha.

Wizara ya Fedha imeandaa  jukwaa la sera na uwekezaji la kuratibu maoni ya wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujadili mustakabali wa uwekezaji, ukusanyaji wa mapato pamoja na ulipaji wa kodi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya amesema jukwaa hilo litafanyika February 27 na 28 mwaka huu jijini Dar es Salama huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kwa niaba ya Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba, tukio Hilo litatoa tathmin ya maoni yaliyokusanywa kutoka kwa watanzania na wadau  mbalimbali yanayohusu marekebisho ya sera ya uwekezaji na kodi nchini " amesema Mwandumbya.

Aidha ameeleza kuwa Wizara ya Fedha ina jukumu la kuratibu upatikanaji wa maoni ya kutoka kwa wadau, kuyachakata na kuyawasilisha katika kamati ya maoni ya kodi ili kuyafanyia tathmini.

Amesema mwezi Juni mwaka Jana2023 Wizara iliandaa jukwaa la wadau wa kodi ambapo maoni yaliyopatikana yalisaidia kwa kiwango kikubwa katika uandaaji wa  bajeti iliyotumika hivi sasa lakini pia yalilenga kukuza uwekezaji, kulinda viwanda vya ndani pamoja na kuvutia wawekezaji.

"National Task Forum ya mwaka jana pia ilikuja na maoni yaliyolenga kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani pamoja na kuongeza pato la serikali" 

Ametaja baadhi ya maeneo  yalofanyiwa maboresho kuwa ni pamoja na kuongeza kimo cha chini Cha usajili wa wafanyabiashara katika kundi la makusanyo ya VAT ambayo yalikuwa milioni 100 na kwa sasa ni milioni 200.

Eneo jingine ni kuanzisha utaratibu wa kufanya maboresho kwenye viwango vya ushuru wa bidhaa Kila baada ya miaka 3 kwa ajili ya utulivu wa kisera, kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye uuzaji wa nyumba mpya zenye thamani isiyozidi shilingi milioni 50.

"Eneo jingine lililofanyiwa maboresho ni kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vifaa vinavyotumika kubadilisha matumizi ya magari kutoka mafuta kwenda umeme na gesi ili kuendana na tabia ya nchi ambayo inaendelea kwa sasa lakini pia ili kukidhi mahitaji ya soko" amesema Mwandumbya.

Amesema zaidi ya  wadau  800 watajumuika pamoja kujadili mustakabli wa uwekezaji na ulipaji kodi na kujadili hali ya uchumi Duniani inavyoenda, na mpango mkakati wa kufanya kuhakikisha uchumi wa Taifa hautetereki.

Ametaja baadhi ya wadau kutoka sekta binafsi  walioshirikiana nao kuwa ni pamoja na Tanzania Private Sectors Foundations (TPSF), Chamber of Tanzania Industry (CTI), Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA), Chamber of Mining na Sekta ya Fedha.

Amesema mada Kuu itakayojadiliwa siku hiyo ni "Mageuzi ya Sera kwa Lengo la Kukuza Uwekezaji, Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani na Kuongeza Ukuaji wa Uchumi Jumuishi"

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post