WALEMAVU WAOMBA KUSHIRIKISHWA VIKAO VYA SERIKALI MTANDAO (e-GA).

*Naibu Waziri Kikwete aagiza (eGA) kuwasaka Matapeli

Na Egdia Vedasto

Arusha 

Chama wa Watu wenye ulemavu wa kusikia Tanzania CHAVITA, kimeiomba serikali na taasisi zake kuwashirikisha kikamilifu katika vikao inavyokuwa ikiandaa ili na wao waweze kutambulika kama ambavyo Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imekuwa ikiwaalika katika mikutano yake inayoiandaa.

Akizungumza katika hafla ya kufunga kikao kazi cha siku tatu kilichoandaliwa na  Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Pwani,  Zalala  Selemani ameshukuru mamlaka hiyo kwa kukubali kuwashirikisha katika vikao inavyoandaa ambapo hadi Sasa  wamepata elimu ya kutosha.

Aidha Ameongeza kuwa watu wenye ulemavu wasibaguliwe wala kuachwa nyuma kwani wako tayari kushiriki kikamilifu vikao vyote vya Serikali pale watakapo alikwa.

Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akifungua mkutano wa nne wa kikao kazi Cha wadau wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Jana Jijini Arusha.

"Tunaziomba taasisi zingine kuiga mfano wa mamlaka ya serikali mtandao kutushirikisha katika vikao na mikutano mbalimbali ili kutuongezea uelewa na ufanisi katika utendaji wa kazi zetu" Ameomba Zalala.

Akifunga kikao  hicho  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya  Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Ridhiwan Kikwete, ameipongeza Mamlaka ya serikali mtandao    kuwashirikisha  watu wenye ulemavu na kuitaka mamlaka hiyo kushirikisha makundi yote ikiwemo watu wasioona na kuboresha matumizi ya nukta nundu.

Licha ya kupongeza juhudi za mabadiliko ya serikali mtandao katika taasisi nyingi za Serikali, Kikwete  ameitaka mamlaka hiyo kupambana na  watu wanaofanya matumizi yasiyo sahihi kimtandao kwa kufanya utapeli jambo ambalo limekuwa likileta taharuki na sintofaham katika jamii.

"Serikali mtandao ni mfumo mzuri utakaorahisisha utoaji huduma katika jamii, lakini Kuna matapeli wanaoumiza watu, Mimi ni mhanga mmojawapo, nimewahi kudanganywa na mtu aliyejifanya ni kiongozi akiomba msaada wa pesa,  baada ya kumtumia niligundua ni tapeli, hili lifanyiwe kazi" amesema Ridhiwani.

Mamlaka ya serikali mtandao imejipanga kutoa tuzo kwa taasisi zitakazofanya vizuri na kuzitambua taasisi ambazo hazitazingatia matumizi sahihi ya serikali mtandao kwani zitakuwa zinarudisha nyuma jitihada za serikali katika utoaji Bora huduma.

Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akimkabidhi tuzo mmoja wa wadau walioshiriki kikao kazi Cha nne Cha wadau wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA ), kilichomalizika Jana Jijini Arusha.

Mkutano huo uliodumu kwa siku tatu umehudhuriwa na zaidi ya Wadau 1300, tofauti na matarajio ya wadau 1000 hapo awali, ambapo washiriki wanatoka katika taasisi mbalimbali za Serikali,  wakiwemo Wakuu wa Taasisi, Maafisa wa TEHAMA, Wakurugenzi na Makatibu tawala. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mhandisi Benedict Ndomba amesema kikao hicho kimemalizika leo tarehe 8Februari 2024, kwa washiriki kuweka maazimio na mpango mkakati wa kuhakikisha taasisi zote serikalini zinajiunga na serikali mtandao.

Washiriki kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo maafisa Tehama na Maafisa Masuhuli wakipiga makofi ndani ya ukumbi wakati Naibu Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete akiwasilisha hotuba yake ya ufungaji wa kikao kazi Cha nne Cha wadau wa Mamlaka ya Serikali Mtandao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post