MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ANAMRINGI MACHA ATOA MAELEKEZO KWA MA DC, WAKURUGENZI NA WATENDAJI IDARA YA ARDHI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, wakurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na watendaji wa idara ya Ardhi kwenda kutatua migogoro ya ardhi kwa wananchi.

Ameyasema hayo leo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karena Hotel baada ya makabidhiano ya nyaraka na ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

RC Macha amesisitiza viongozi hao kwenda kutatua changamoto za ardhi ana kwa ana huku akiwahimiza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu mipaka na haki zao katika umiliki wa ardhi na kwamba hatua hiyo itasaidia kuimarisha usalama kwa wananchi.

“Yapo masuala ya migogoro ya Ardhi tukajipange kwenye Halmashauri na mashauri yetu yanayohusu Ardhi ni vizuri tukaenda kuyafanyia kwenye eneo linalozozewa tusiende ofisini kufanya maamuzi, sidhani kama tutaimaliza migogoro ya Ardhi kwa kutatua tukiwa ofisini hiyo tutadanganyana nafikiri ofisi zetu za idara ya Ardhi ziwe zinaenda kuweka kambi kwenye maeneo yenye changamoto ili kutatua migogoro hiyo”.  Amesema RC Macha

Amewataka wakurugenzi wa Halmashauri, wenyeviti wa Halmashauri pamoja na wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia vema suala la ukusanyaji wa mapato ili kuepusha changamoto mbalimbali ikiwemo wizi ambapo amesema kuimarika kwa zoezi la ukusanyaji wa mapato itasaidia kwa kiasi kikuwa kuchochea maendeleo.

Amesema serikali itaendelea kuwahakikisha mazingira ya Amani,usalama na upatikanaji wa huduma bora na stahiki za kijamii wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Kwa upande naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki  vema kwenye ajenda ya kitaifa ya  matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira.

 “Niwaombe wana Shinyanga katika ajenda hii ya mazingira ifikapo Mwaka 2030 wanawake asilimia 88 wawe wanatumia nishati safi ya kupikia lakini pia tuwe wa kwanza katika suala la utunzaji wa mazingira lakini tuendelee kumuunga Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala hili la utumiaji wa nishati safi ya kupikia na utunzaji wa mazingira”.amesema Mndeme

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga mpya Mhe. Anamringi Macha leo amekabidhiwa ofisi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake ambapo amejitambulisha kwa viongozi mbalimbali hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hotel mjini Shinyanga na kwamba siku chache zimepita baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza kwenye hafla hiyo leo Jumatatu March 18,2024 katika ukumbi wa Karena hotel mjini Shinyanga.

Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi. Christina Mndeme akizungumza kwenye hafla hiyo leo Jumatatu March 18,2024.

 

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batibayo akizungumza kwenye hafla hiyo.




This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post