SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA KATIKA MAPAMBANO YA VITENDO VYA UKATILI

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kampeni ya kupinga ukatili Nchini SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imeiomba Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuendelea kushirikiana ili kupunguza au kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika jamii.

Hayo yamebainishwa  na viongozi wa SMAUJATA katika kikao cha pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kilicholenga kuwatambulisha viongozi wa SMAUJATA Halmashauri hiyo.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya pamoja na Mwenyekiti idara ya itifaki, uachama na uenezj Bwana Solomon Najulwa wameomba ushirikiano kati ya SMAUJATA na viongozi wa Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bwana Daniel Joseph pamoja na Katibu wa SMAUJATA Halmashauri hiyo Bi. Nives Nyoni wameahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii ili kufikia malengo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge amesema Serikali ya Halmashauri hiyo itatoa kushirikiana ili malengo ya kampeni hiyo yaweze kutimia.

Shujaa wa Maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini yenye kauli mbiu isemayo Kataa ukatili wewe ni shujaa, kampeni hiyo inatekeleza majukumu yak echini ya Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Mwenyekiti idara ya itifaki, uachama na uenezj Bwana Solomon Najulwa akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao hicho.

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post