Na Mapuli Kitina Misalaba
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga limekumbusha wakala wa barabara za vijijini na mjini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga kushughulikia haraka changamoto ya barabara inayozuia kupita Gari la kupeleka taka kwenye dampo.
Hayo yamebainisha leo Aprili 29,2024 kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga baada ya Diwani wa kata ya Kolandoto Mhe. Mussa Elias kuibua kero hiyo wakati wa maswali na majibu ambapo amehoji kuwa ni lini Gari la taka litaanza kutoa taka kwenye Guba kupeleka kwenye dampo.
Diwani huyo amesema ipo changamoto ya taka kutozolewa kwa wananchi katika kata ya Kolandoto ambapo amesema ni muda mrefu Gari la kuzoa taka halionekani katika huduma hiyo.
“Nimekuwa nikihoji mara nyingi sana kuhusu Guba katika kata ya Kolandoto hali ni mbaya sana kwa kipindi hiki hasa wakati wa Mvua hizi zinazoendelea, nataka kujua leo mkurugenzi anampango gani kuhusu Guba la taka hasa kwenye kata yangu ya Kolandoto kwa sababu mpaka sasa hivi Guba limejaa na alizoewi”.amesema Diwani Mhe. Mussa
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocutus Litundu ametolea ufafanuzi huku akikili kuwepo kwa changamoto hiyo.
“Kwanza nikili kwa sasa hivi tunachangamoto kubwa si kata tu ya Kolandoto hii changamoto ipo takribani mji wetu wote hii changamoto ya uzoaji taka ipo, sababu kubwa inayokwamisha tunachangamoto ya barabara yetu inayokwenda kule dampo wakati mwingine magari yanashindwa kufika kule kwa ajili ya ubovu wa miundombinu ya barabara lakini juhudi na hatua mbalimbali zimeshachukuliwa na uongozi kwahiyo changamoto hiyo inashughulikiwa”.amesema Litundu
Mwakilishi kutoka TARURA Wilaya ya Shinyanga amesema tayari maboresho katika hatua mbalimbali kwenye barabara hiyo yanaendelea ili Gari la taka liweze kupita.
“Sisi kama TARURA wiki iliyopita tumefanya matengenezo katika hilo barabara kwa kufukia mashimo yote lakini kuna maeneo kama mawili hivi bado yana changamoto ambayo bado yanahitaji kuboreshwa zaidi lakini sehemu kubwa ambayo ilikuwa na maeneo yenye shida tumepeleka mtambo na magari maboresho yanaendelea”.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuka pamoja na mambo mengine amesisitiza changamoto ya barabara kutatuliwa kwa haraka ili Gari la taka liweze kupita.
Mhe. Masumbuko ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kuendelea kuzingatia suala la usafi wa mazingira ili kuepukana na athari mbalimbali ikiwemo mlipuko wa magonjwa.
“Mimi mwenyewe niliondoka kwenda kuona ile changamoto ya barabara ni kweli hakukuwa na mazingira rafiki ya kupitisha takataka na hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa tuamini tu kwamba hali ya hewa ikikaa vizuri mkandarasa aliyepewa hiyo kazi atakamilisha lakini takataka zipo nyingi hapa mjini kwa sasa hata mimi leo pia nimepigiwa simu stendi yetu ya Manyoni takataka zimejaa sana hata yale maji machafu na menyewe yanakwenda kule kule kwenye dampo kwahiyo changamoto hiyo bado ni kubwa na sisi tu tuhimize mazingira ya usafi yaendelee na watu wachukue tahadhari ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko”.amesema Mhe. Masumbuko
Kwa upande wake Naibu meya wa Manispaa ya Shinyanga Zamda Shaban amesema suala la uzoaji wa taka katika maeneo ya watu ni muhimu hivyo naye amesisitiza mkurugenzi kwa kushirikiana na TARURA kuharakisha maborsho ya barabara ili Gari la taka liweze kupita ili kuondoa usumbufu unaojitokeza katika jamii.
Katika mkutano huo wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga madiwani kutoka kwenye kata husika wamewasilisha taarifa zao za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo huku wakitaja changamoto zilizopo.
Moja ya changamoto zilizotajwa leo kwenye mkutano huo ni upungufu wa walimu kwenye badhi ya shule za msingi na sekondari ambapo wamemkubusha mkurugenzi kushughulikia changamoto hiyo ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Aidha imebainishwa changamoto ya upungufu wa matundu cha choo katika shule ya msingi Mapinduzi B iliyopo kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ambapo idadi ya wanafunzi ni zaidia ya 4000 pamoja na walimu katika shule hiyo hawana vyoo.
Pia madiwani hao wamesema bado ipo changamoto ya upungufu wa watumishi hasa watendaji wa mitaa katika kata mbalimbali ikiwemo kata ya Ngokolo, Mjini, Lubaga na Chibe Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Chibe Mhe. Kisandu John amesema ipo changamoto ya ufinyu wa chumba cha kujifungulia aki mama katika Zahanati ya Chibe ambapo amesema kipo chumba kimoja tu huku akieleza kuwa Zahanati hiyo inahudumia kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga pamoja na kata za Halmashauri ya Shinyanga vijijini ameomba katika Zahanati hiyo kuongezwa chumba pamoja na vitanda ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Anord Makombe amezungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyia Mwaka huu ambapo amesema ni muhimu kila mmoja kujiandaa na uchaguzi huo ili kuhakikisha kila mtaa anapatikana kiongozi bora.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuka akizungumza leo Aprili 29,2024 kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa za kwenye kata kutoka kwa madiwani wa kata husika.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza leo Aprili 29,2024 kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa za kwenye kata kutoka kwa madiwani wa kata husika.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Revocutus Litundu akizungumza kwenye baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Aprili 29,2024.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Anord Makombe akizungumza leo Aprili 29,2024 kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa kutoka kwa madiwani wa kata za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale akizungumza kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Diwani wa kata ya Kizumbi Mhe. Reuben Kitinya akizungumza kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Diwani wa kata ya Mwamalili Mhe. James Mdimi akizungumza kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Diwani wa kata ya Masekelo Mhe. Pitter John akizungumza kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Diwani wa kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akizungumza kwenye mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Diwani wa viti maalum kata ya Ngokolo akiwasilisha taarifa ya kata hiyo kwenye baraza la madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 leo Jumatatu Aprili 29,2024.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye kata mbalimbali likiendelea leo Aprili 29,2024.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye kata mbalimbali likiendelea leo Aprili 29,2024.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkutano wa robo ya tatu 2023/2024 wa kupokea na kujadili taarifa kutoka kwenye kata mbalimbali likiendelea leo Aprili 29,2024.