SHEIKH WA MKOA WA SHINYANGA ISMAIL MAKUSANYA ATOA WITO KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KUWA CHAHU YA AMANI NA UTULIVU KATIKA SIKUKUU YA IDD EL FITRI

 

TAZAMA VIDEO VIONGOZI WAKIZUNGUMZA.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya ametoa wito kwa waumini wa dini ya Kiislam Mkoani Shinyanga kutumia sherehe za Idd El Fitri kuchagiza amani na utulivu kwa watu wote hasa wenye mahitaji.

Akitoa salamu za Idd El Fitri baada ya swala iliyofanyika katika uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga Sheikh Makusanya amesema ni wajibu wa waumini hao kuwa chanzo cha faraja na amani kwa jamii nzima akiwataja wagonjwa, wafungwa na watu wengine wenye uhitaji .

Amehimiza kutembelea wafungwa, wagonjwa na wale wote wanaohifadhiwa kwenye vituo vya kulelea ili kuwapa faraja na amani kiroho na kimwili.

“Kwa wewe ambaye ulipata kufunga mwezi mtukufu wa ramadhan tunatarajia watu wapate manufaa kutoka kwako watu wapate amani kutoka kwako lakini pia kwa wale ambao wako makabulini wewe utakwenda makabulini kuwaombea dua lakini kwa ndugu zetu ambao wamefungwa wewe uende kule uwape faraja uende kule uwaombee dua uwape chakula lakini vile vile wale ndugu zote tulionao waislam na wasiokuwa waislam tujumuike nao pamoja, kwahiyo wewe kama wewe iwe ni sehemu ya kuleta amani na utulivu tuwe ni watu wa kuhurumiana hasa katika siku hii ya leo”.amesema Sheikh Balilusa

Kwa upande wake kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri BAKWATA Mkoa wa Shinyanga Sheikh Khamis Balilusa amewakumbusha waumini wa Dini ya kiislam kuendelea kuwa mfano wa matendo mema na kutojihusisha na vitendo vinavyokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

“Waislam wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga watambue siku hii ni siku tukufu ni siku ambayo tunapaswa sisi waislam kutekeleza wajibu wetu wa kushirikiana kutembeleana na kusaidiana pia tunapaswa tuhakikishe wale wajane watoto yatima tunawaona na kuwajali ili wapate furaha hasa siku ya leo lakini pia nitumie fursa hii kuiomba jamii kwamba tujifunze yale yote yaliyofanyika mwezi mtukufu wa ramadhan kuzidisha wema lakini pia kuhakikisha sisi waislam kuonya na kujiepusha na tabia mbaya za manyanyaso katika jamii yetu mauaji mateso kwa watoto na akin a mama pamoja na ubakaji hivi ni vitu ambavyo waislam naomba wawe kipaumbele kuvisimamia ili kuufanya mji wetu uendelee kuwa salama na pia uendelee kuwa mji wa amani”.amesema Sheikh Balilusa

Misalaba Media imezungumza na baadhi ya waumini wa Dini ya kiislam baada ya swala ya Idd al Fitri ambao wameahidi kuendeleza utu wema na matendo mema.

Leo ni siku ya Idd al Fitri ambapo watanzania wameungana na wenzao Duniani kote kusherehekea sikukuu hiyo baada ya kuhitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza swala kwenye ibada ya Idd El Fitri ambayo imefanyika katika uwanja wa Saba saba Kambarage mjini Shinyanga leo Aprili 10,2024.


 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post