Rais Mwinyi Mgeni Rasmi mkutano wanahisa CRDB

Wajumbe wa Bodi ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja huku wameshikilia ripoti ya ukaguzi ya Mwaka 2023/2024

 Seif Mangwangi

Arusha

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa semina ya wanahisa  wa benki ya CRDB kesho Jijini Arusha.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Ally Laay Mkutano huo wa wanahisa utafuatiwa na Mkutano Mkuu wa 29 utakaofanyika Jumamosi  Mei18, 2024 katika kituo Cha Mikutano Cha Kimataifa AICC.

Amesema katika mkutano huo mambo mengi yatajadiliwa ikiwemo fursa mbalimbali zilizopatikana kwa mwaka mzima ikiwemo utoaji wa gawio la Shilingi Milioni 130.6 kwa wanachama ambapo kila mwanahisa anaenda kupata gawio la Shilingi 50.

" Benki yetu imekuwa na mafanikio mengi sana ikiwemo kupunguza mikopo chechefu kwa asilimia tatu  hii inatokana na usimamizi mzuri wa mikopo hiyo lakini pia utaona gawio la hisa limepanda hadi kufikia  Shilingi 50 mwaka huu 2024 sawa na asilimia 34 kutoka gawio la Shilingi,45 mwaka jana,".

Amesema CRDB imepata  faida ya bilioni 428.8 kwa mwaka 2023 kutoka bilioni 351 .4  mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 21 baada ya kodi.

" Baada ya kupata faida hii, bodi ya wakurugenzi imependekeza gawio la Shilingi 50 kwa hisa, sawa na ongezeko la asilimia 11.11 ikilinganishwa na gawio la Shilingi,45 lililotolewa mwaka 2022," amesema.

Amesema iwapo pendekezo hilo litaidhinishwa katika mkutano mkuu wanahisa wataweza kuvuna gawio la Shilingi bilioni 130.6  sawa na asilimia 34 ya faida halisi ikiwa ongezeko la bilioni 117.5 lililolipwa mwaka 2022.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki ya CRDB Dkt Ally Laay akionyesha kitabu chenye taarifa ya ukaguzi wa mahesabu ya benki hiyo ambayo inaenda kuwasilishwa kesho kwa wanahisa wa benki hiyo

Dkt. Laay  amesema katika kutafuta fursa zaidi za ufanisi wanatarajia kufungua matawi zaidi ya benki hiyo katikanchi za Zambia,Uganda  na visiwa vya  Comoro.

Mkurugenzi wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela amesema benki hiyo inarudisha fadhila kila mwaka kwa jamii ikiwemo kutoa mikopo kwa vijana mashuleni ,vyuoni na Mitaani  kwaaajili ya bunifu na gunduzi mbalimbali  ili kuwasaidia mawazo yao kuboreshwa zaidi sanjari na kupewa mikopo itakayowasaidia kuwainua kiuchumi kupitia bunifu zao.

Wajumbe wa Bodi ya CRDB 

Amesema benki ya CRDB itaendelea kuwainua wanawake, vijana na makundi mbalimbali kiuchumi kwa kuwapatia  mikopo nafuu sanjari na kuwezesha mawakala wanaotoa huduma za kifedha kuboresha huduma za mtandao pamoja na kufungua matawi mengi zaidi kwaajili ya utoaji huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia za hali ya juu.

"CRDB tumekuwa tukitenga asilimia 1 ya faida ambayo tumekuwa tukiipata kwa mwaka na kuirejesha  kwa jamii na hapa tumekuwa tukichangia shughuli mbalimbali kama elimu, majanga, mazingira na zaidi  kuwajengea uwezo wanawake na vijana kupata mikopo ili  kujikwamua kiuchumi,"Amesema.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post