WAANDISHI WA HABARI MITANDAONI WATAHADHARISHWA NA HABARI ZA UCHOCHEZI

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAANDISHI wa habari mitandaoni wametakiwa kuepuka kuandika habari za uchochezi na ambazo zimekiwa zikivuruga amani ya nchi kwa lengo la  kupata wasomaji wengi na kujikuta wakiingia kwenye mgogoro na vyombo vya Sheria.

Akizungumza kwenye kongamano la  Jumuiya ya wanahabari mitandaoni (JUMIKITA), linaloendelea Leo Mei21,2024 katika ukumbi wa maktaba ya Chuo kikuu cha Daar es Salaam,  Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime amewataka waandishi kuchambua habari kabla ya kuandika.

Amesema ulinzi na usalama wa Mwandishi wa habari ni muhimu sana kuzingatiwa lakini wanahabari wanatakiwa kufuata Sheria, kanuni na misingi ya habari.

" Lazima mzingatie Sheria mbalimbali za habari, msiandike habari tu kwa kuwa ni habari, mkizingatia hizi Sheria tutaweza kuwa na mitandao mizuri itakayotupatia habari nzuri katika jamii,"amesema.

Ameutaka uongozi wa JUMIKITA kusaidia kutoa elimu kwa wanahabari mtandaoni ili kudhibiti hali hiyo kama ambavyo Baraza la habari Tanzania limekuwa likifanya.

" Mataifa ya wenzetu waandishi wao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutangaza mataifa yao, na sisi lazima tuwe wazalendo, tutangaze Taifa letu na kulitetea kwa namna yoyote Ile," Amesema Misime.

Kwa upande wake Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mkurugenzi wa Leseni katika Mamlaka hiyo, John Daffa amesema Tanzania ina watumiaji wa internet Milioni 36 pamoja na vifaa ya kutumia internet milioni20.

Amesema tukitumia majukwaa haya ya habari vizuri pamoja na mitandao kuna fursa nyingi ambazo zinaweza kuingiza kipato.

John Daffa amesema kama wanahabari mtandaoni wanapaswa kuzingatia usalama ikiwemo kufungua link ambayo hawaifahamu sanjari na kutumia nywila ambayo ni ngumu mtu mwingine kuweza kuifahamu kirahisi.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post