DC MTATIRO ATOA MAGIZO KWA WATENDAJI NA WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI

 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitoa maagizo kwa watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwenye maeneo yao.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro amewataka watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na matumizi ili wananchi waweze kujua changamoto na mafanikio katika maeneo yao.

Ametoa agizo hilo wakati akisikiliza kero na malalamiko mbalimbali katika mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Solwa pamoja na mambo mengine wamesema ipo changamoto ya  mtendaji na mwenyekiti wa kijiji hicho kutosoma taarifa za mapato na matumizi kwa muda mrefu.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji, wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na matumizi ili kuepusha mikanganyiko kwa wananchi hasa katika miradi inayoendelea kutekelezwa kwenye maeneo yao.

DC Mtatiro pia amewasisitiza watumishi wote wa serikali ambao wapo chini yake kutekeleza majuku yao kwa weledi kwa kuhakikisba wanatoa huduma bora kwa wananchi.

“Sisi tumepewa hizi kazi tumepewa na vifaa tunaofisi kila kitu tumepewa kazi yetu ni kuwahudumia wananchi tunatakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi ndiyo maana nawaomba wasaidizi wangu watu wote wanaofanya kazi chini yangu kuanzia kwa mkurugenzi mtendaji, watumishi wengine ambao wapo chini yake, magavana, watendaji wa kata na watu wote wanaotoa huduma kwa wananchi huu wakati wangu nikipata malalamiko yanayomhusu mtendaji yoyote wa dawati la serikali ambaye hawahudumii wananchi ipasavyo moto wake ni mkubwa na moto utawaka kweli kweli”.amesema DC Mtatiro

Katika mkutano huo wa hadhara wananchi wametaja kero na malalamiko mbalimbali ikiwemo changamoto ya ukusanyaji wa ushuru wa mazao pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara huku DC Mtatiro akimtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kushirikiana na wataalam wake katika kutatua kero na changamoto zilizopo.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali amesema Halmashauri hiyo itaendelea kushughulikia kwa uharaka changamoto zilizopo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro ameendelea na ziara zake kutembelea kila kata kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi ambapo amewasisitiza wananchi kuwasiliana naye  pale wanapobaini changamoto kwenye maeneo yao ili iweze kutatuliwa kwa uharaka.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. 

Mkutano wa hadhara kata ya Solwa ukiendelea ambapo lengo la mkutano huo ni mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatirokatika kusikiliza na kutatua kero za wananchi.








This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post