MAADHIMISHO SIKU YA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WAZEE 2024 YAFANYIKA KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA

 

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akisoma taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Serikali itaendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yote ya kata  17 za Manispaa ya Shinyanga.

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko wakati akisoma taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.

Amesema itaendelea na uboreshaji wa huduma za kijamii ikiwemo kutoa elimu bila malipo na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo mbalimbali  ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwa wazee kutembea ubali mrefu kufuata huduma hizo.

“Tutaendelea na uboreshaji wa huduma za kijamii ikiwemo kutoa elimu bila malipo na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yetu ili wazee wetu wasitembee umbali mrefu kupata huduma hizo kama mnavyoona katika serikali yetu ya awamu ya sita imeendelea kujenga na kuboreshaji huduma za kutolea huduma za afya ambapo karibia kata zote katika Halmashauri yetu zinavituo vya kutolea huduma za afya”

“Nimtake  mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na wizara za TAMISEMI na wizara ya Afya kuimarisha upatikanaji wa dawa na wataalam wabobezi wa magonjwa ya wazee hususan kwenye Hospitali zetu za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuhakikisha kundi hili muhimu linatambuliwa na kupewa kapaumbele ikiwa ni pamoja na kupatiwa vitambulisho au kadi za matibabu ya wazee”.

“Kuhusu suala la tiba kwa wazee serikali imeunda kamati maalum kwa ajili ya kuleta mapendekezo serikalini kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hii, wakati serikal ikiendelea kupitia mapendekezo ya kamati hiyo nataka niwaahidi wazee wangu kuwa yale yote yanayowafanya wazee kuwa kwenye kundi hatarishi tutayashughulikia”

“Kwa ujumla changamoto na maombi yote mliyoyawasilisha niya msingi hivyo basi serikali tumeyapokea na tutajitahidi kuyashughulikia na kwa bahati nzuri masuala yote mliyoyaeleza yapo kwenye ilani yetu  ya uchaguzi ya 2020\2025 na pia tumeyajumuisha kwenye mpango wa tatu wa taifa wa maendeleo kwa Miaka mitano ambayo utekelezaji wake tuliuanza Mwezi Julai 2021”.

Kupitia taarifa hiyo pia amewasisitiza wazee kuendelea kuhimiza malezi bora kwa watoto pamoja na kudumisha amani na usalama ili kuendelea kujenga taifa bora.

“Niwakumbushe wazee kuendelea kuhimiza malezi bora kwa watoto ili kujenga taifa la watu waandilifu, waaminifu, na wazalendo kwa nchi yao wasio jihusisha na vitendo viovu vya wizi, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine ambavyo ni kinyume cha maadili na tamaduni zetu “.

“Kama mnavyofahamu amani na usalama ni msingi wa maendeleo bila ya amani hakuna  maendeleo na zaidi pasipo na amani wenye kuathirika zaidi ni pamoja na wazee hivyo wazee wangu tunalojukumu kubwa la kuhakikisha tunadumisha amani katika Wilaya yetu”.

“Kapaumbele kingine ni kulinda uhuru, muungano wetu na mshikamano mambo haya hayana mbadala hivyo tutaendelea kuyaenzi, kuyatunza na kuyaendeleza pili kuendeleza jitihada za kukuza uchumi na hapa tunaendeleza kazi nzuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafiri na huduma za usafirishaji lengo ikiwa ni kuchochea ukuaji wa uchumi nchini”.

Awali akisoma risala, mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano amesema baraza hilo linaendelea kukemea kila aina ya ukatili kwa wazee ikiwemo ukatili wa kutelekezwa na familia zao.

“Ukatili kwa wazee upo katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na mauaji ya vikongwe, kutelekezwa wazee na familia, kunyimwa fursa ya maendeleo ya kiuchumi na kutoheshimiwa wazee kwenye nafasi za huduma mbalimbali tamko letu sisi wazee sehemu zote za kutolea huduma ni mzee kwanza jambo la pili waganga na wauguzi wanajitahidi kuwapa huduma wazee wetu kwa kidogo kinachopatikana”.amesema mzee Tano

Kwa upande wake mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert amesema tayari ipo ratiba ya wataalam wa afya kupita kila kata kwa ajili ya zoezi la upimaji ili kutambua hali za afya kwa wazee.

“Tutakuwa na ratiba ya kupita kila kata angalau kila Mwezi mara moja tutakuwa tunaifikia kata moja kwa ajili ya kuwafikia wazee wote walipo ili waweze kupata hizi huduma ambazo zinaendelea hapa tunafanya hivo kwa sababu sasa hivi tatizo linalowakumba wazee ni ugonjwa wa shinikizo la damu”.

“Ukienda katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa tunapokea wagonjwa ambao  wanakiharusi yaani ambao wanapoteza nguvu sehemu moja ya mwili yaani mmoja wawili hadi wane ndani ya masaa 24 hii hali inatokea kwa sababu wengi hatutambui afya zetu, tunatembea tunafanya kazi lakini hatutambui afya zetu kwahiyo tukianza hii kampeni ya kupita kila kata wazee wote watapata nafasi ya  kutambua afya zao na watakapokuwa wametambua afya zao sisi kwa upande wa idara ya afya kazi yetu ni kuwahudumia wazee na ndiyo kipaumbele chetu”.amesema Dkt. Elisha

Maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee kwa Mwaka huu 2024 yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga na kwamba yamehudhuriwa na wazee wenye umri kuanzia Miaka 60, viongozi mbalimbali wa serikali, wadau pamoja na viongozi wa mabaraza ya wazee katika ngazi ya kijiji, mtaa, kata na Manispaa ya Shinyanga.

Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo upimaji wa afya kwa wazee, utoaji wa elimu ya kujikinga magonjwa yasiyoyakuambukiza pamoja na elimu ya kupambana na ukatili kwa wazee.

Katika huduma zilizotolewa  juu ya magonjwa yasiyoyakuambukiza ni pamoja na kupima presha, Sukari na magonjwa ya moyo pia wataalam wa afya wametoa ushauri kwa wazee hao juu ya kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambukiza pamoja na namna ya kuishi kwa wale wenye matatizo hayo.

Lakini pia umetolewa ushauri nasaha juu ya lishe bora kwa wazee ikiwa ni pamoja na matibabu sahihi na kujitokeza katika follo- up kwa wenye matatizo hayo inayofanyika kila siku ya Alhamisi katika kituo cha afya Kambarage.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ni kila Mwaka ifikapo Juni 15 ambapo  kwa Mwaka huu 2024 katika Manispaa ya Shinyanga kauli mbiu inasema “WAZEE WA SHINYANGA TUPAZE SAUTI TUYADUMISHE MAADILI MEMA”

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.

Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akisoma risala ya baraza hilo katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.

Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akikabidhi risala kwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024 ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024 ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.

Afisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.

Viongozi mbalimbali.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post