MKURUGENZI WA THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION BWANA PETER FRANK (MR. BLACK) AWAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KWENYE TAMASHA LA UTAMADUNI WA MSUKUMA NHELEGANI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kuelekea tamasha la utamaduni wa Msukuma Shinyanga, taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION imefanikisha marekebisho ya kupaka rangi katika jengo la ofisi ya Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga.

Akizungumza Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) amesema tamasha la utamadun wa Msukuma hufanyika kila Mwaka na kwamba kabla ya tamasha hilo hufanyika shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii.

Mr. Black ameelezea zaidi kuwa Mwaka huu 2024 pamoja na mambo mengine imefanyika shughuli ya kuboresha jengo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga kwa kupaka rangi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuelekea kilele cha SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3.

Mkurugenzi huyo Mr. Black amesema pamoja na maboresho katika jengo la Mahakama ya Mwanzo mjini, taasisi THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kwa kushirikiana na serikali imepanda miti zaidi ya 30 katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira.

“Kupitia tamasha hili kila Mwaka tumekuwa tukiandaa shughuli mbalimbali kabla ta tukio husika ukijaribu kuangalia Miaka ya nyuma kuna mambo mbalimbali ya kijamii ambayo tumeyafanya ikiwemo marekebisho ya miundombinu mbalimbali lakini pia uwezeshaji katika sehemu mbalimbali na Mwaka huu tumejikita kurekebisha jengo la Mahakama ya mwanzo ya mjini kulikuwa na uchakavu kidogo wa kuta za nje upande wa rangi tukaona ni vyema sisi wadau wa maendeleo Mkoa wa Shinyanga tuweze kuweka mkono wetu kufanikisha jambo hili ikiwa ni shukurani yetu na sadaka yetu kuelekea tamasha la utamaduni wa Msukuma”.

“Asili yetu ni uwoto wa asili tumeshiriki pia katika kupanda miti ambapo tumepanda miti zaidi ya 30 katika eneo linalozunguka Mahakama hii kwa lengo la kutengeneza kivuli na miti ya matunda lakini pia kuuendeleza uwoto wa asili wa Mkoa wa Shinyanga”.amesema Mr. Black

Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahora ameishukuru taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION huku akimpongeza Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kufanikisha ukarabati wa jengo la Mahakama ya mwanzo mjini kwa kupaka rangi.

“Sisi tunashukuru sana kuwa sehemu ya wanufaika wa tamasha la utamaduni wa Msukuma lakini kwa dhati kabisa niishukuru kampuni hii ya  BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kupitia mkurugenzi wake Bwana Peter Frank alimaarufu MR. BLACK kwa safari hii kutuona na sisi Mahaka ya Wilaya ya Shinyanga kuwa wanufaika wa tamasha hili kwa kupaka rangi jengo hili limependeza kwahiyo tunashukuru sana, kwa niaba ya uongozi wa Mahakama ndani ya Wilaya ya Shinyanga tunaahidi kabisa ushiriki wetu usiokuwa wa mashaka tutakuwa wote katika tamasha mwanzo mpaka siku ya mwisho”.amesema Zahora

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga naye ameipongeza taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kwa ubunifu wao katika shughuli za kijamii ambapo amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika shughuli hasa za kijamii zinazogusa sekta mbalimbali hasa katika kulina na kuendeleza utamaduni wa Mkoa wa Shinyanga.

Naye mhifadhi misitu wa Wilaya ya Shinyanga kutoka taasisi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Bwana Fabian Balele ameipongeza taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kwa kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uhifadhi wa misitu ambapo amesema TFS itaendelea kushiriki kikamilifu katika tamasha la utamaduni wa Msukuma.

Tamasha la utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3, ambalo limeandaliwa na THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Mwaka huu 2024 litafanyika kwa siku mbili kuanzia Jumamosi Juni 29 hadi Jumapili Juni 30.

Mr. Black ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau na wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi ambapo amesema yatafanyika maonyesho ya Biashara, sanaa, ngoma za asili, burudani pamoja na Nyama choma”.

Tamasha hilo la utamaduni wa Msukuma litafanyika katika viwanja vya Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kwamba hakuna kingilio  “SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3, LEJIGUKULU LYA NZENGO”.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kufungua tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumamosi Juni 29,2024.

Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Suleiman Serera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kufunga tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumapili Juni 30,2024.

Kauli mbiu ya tamasha la utamaduni wa Msukuma kwa Mwaka huu inasema “UTAMADUNI WETU URITHI WETU, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA”


 

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post