MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILKI ZA ARDHI KUANZA JULAI MOSI 2024 HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo imefanya mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi unaotarajiwa kuanza utekelezaji wake Julai mosi Mwaka huu 2024 kwenye kata 9 za Halmashauri hiyo katika awamu ya kwanza.

Mgeni rasmi katika mkutano huo ni katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akimwakilisha mkuu wa Wilaya hiyo Wakili Julius Mtatiro.

Wakati akifungua mkutano huo Bwana Kitinga pamoja na mambo mengine amewasisitiza wasimamizi wa mradi huo kutekeleza majukumu yao kwa weledi, haki na usawa ili kuepusha migogoro kwa wananchi.

Pia amehimiza wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambao watafikiwa  na mradi huo kutoa ushirikiano ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa katika kuimarisha Wizara ya Ardhi.

‘Nawaomba mchukue kama fursa kwenu na kutoa ushirikiano thabiti ili kufanikisha utekelezaji wake, maeneo mengi yalitamani kupata fursa hii lakini kutokana na uchache wa rasilimali hawakufanikiwa kufikiwa na mradi’.

“Nashauri itumieni fursa hii kikamilifu kwa maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Mkoa wetu wa Shinyanga kwa ujumla, uboreshaji wa milki wa Ardhi katika Wilaya utaleta matokeo chanya katika kuchochea maendeleo ya Wilaya ikiwa ni pamoja na kuleta usalama wa milki za Ardhi, kukuza uchumi na kupunguza au kumaliza migogoro itokanayo na Ardhi”.

“Mtakaopata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi huu kwa kufanya au kushauri serikali, nawaomba mfanye kazi kwa uaminifu na uadilifu wa hali ya juu kwa kuzingatia uzalendo (Taifa kwanza) nawaomba wote tuwe wamoja tusemezane ndani kwa ndani tuyarekebishe yale ambayo yanaweza kutia dosari katika mradi lakini pia msifumbe macho wala kusita kuwasiliana na ofisi yangu kwa mambo yanayohitaji kuboreshwa ili kuifanya Halmashauri yetu kupata matokeo chanya”Amesema Kitinga

“Nafurahi kutamka kuwa mkutano huu wa wadau wa mradi wa kuboresha usalama wa milki za Ardhi Nchini unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga nimeufungua rasmi”.

Kwa upande wake afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi ameeleza hatua mbalimbali za utekelezaji mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo amesema kwa awamu ya kwanza kata 9, vijiji 15 na vitongoji 21 vitanufaika na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi.

Bwana Kitosi amesema mradi huo pia utakwenda sanjari na utatuzi wa migogoro ya Ardhi ambapo ameeleza kuwa mradi huo utasaidia kuimarisha makazi yasiyorasimi pamoja na kuongezeka usalama wa miliki katika jamii.

Katika mkutano huo yamefanyika majadiliano ya pamoja ambapo Afisa maendeleo ya jamii Bi. Tumaini Setumbi ametaja baadhi ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo.

“Azimio la kwanza ni utekelezaji wa mradi uanze mapema ili elimu iliyotolewa isisahaulike azimio la pili ni wananchi kupewa elimu zaidi kuhusu umiliki wa ardhi katika maeneo yenye madini lakini pia azimio lingine ni mradi kuajili vijana waliomaliza vyuo walioko katika maeneo yanayofikiwa na mradi” ametaja Setumbi

Bi. Setumbi awali wakati akiwasilisha yake ya usimamizi wa masuala ya mazingira na jamii amesema katika mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi zipo miongozo mbalimbali ili kuhakikisha kuwa masuala ya mazingira na jamii yanazingatiwa ambapo pia amesema upo mpango wa kutambua makundi maalum.

Mradi huu umelenga kuboresha usalama wa milki za Ardhi kwa kupanga, kupima na kusajili milki za Ardhi zipatazo 2.5 zinazojumuisha hati milki 1,500,000 na leseni za makazi 500,000 katika maeneo ua mijini na hati za hakimiliki za kimila 500,000 vijijini ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inakusudiwa kutoa hati milki zipatazo 62,200 katika maeneo ya vijiji 15.

Mradi huu pia umelenga kusimika mfumo unganishi wa kielekroniki wa kuhifadhi kumbukumbu za Ardhi (ILMIS) katika ofisi zote za Ardhi za Mikoa za Halmashauri mbalimbali.

Tanzania inajumla ya Halmashauri 185 kati ya Halmashauri hizo, Halmashauri zaidi ya 60 zinazotarajiwa kunufaika na mradi huu mjini na vijijini ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni miongoni mwa wanufaika katika mradi huo.

 Baadhi ya kata ambazo zitanufaika na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ni pamoja na kata ya Samuye, Isela, Tinde, Didia, Solwa, Salawe, Mwakitolyo, Iselemagazi, Mwenge pamoja na kata ya Usanda.

Mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi umehudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi binafsi, viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, wawakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Shinyanga, madiwani wa Halmashauri hiyo kutoka kata mbalimbali, wakuu wa divisheni na vitengo, wataalam kutoa Wizara ya ardhi makao makuu, wawakilishi wa makundi maalum, viongozi wa kimila na wazee maarufu.

Mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.

Mgeni rasmi, katibu tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bwana Said Kitinga akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.

Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mara ya  hatua mbalimbali za utekelezaji mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa awamu ya kwanza, leo Juni 28,2024.

Afisa mipango miji akimwakilisha meneja urasimishaji mjini, Bwana Paulo Kitosi akiwasilisha mara ya  hatua mbalimbali za utekelezaji mradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa awamu ya kwanza, leo Juni 28,2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje awali akitoa salamu zake katika mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini Mhe. Edward Ngelela awali akitoa salamu zake katika mkutano wa wadau wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo Juni 28,2024.


 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post