MADIWANI VITI MAALUM SHYDC WAANZA ZIARA KUHAMASISHA WANACHAMA WA CCM NA JUMUIYA ZAKE KUSHIRIKI VEMA UCHEGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024

Na Mapuli Kitina Misalaba

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Julai 9,2024 wameanza ziara yao kutembelea tarafa tatu za Halmashauri hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanawake na wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na jumuiya zake kushiriki vema katika hatua zote za uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024.

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga inajumla ya kata 26 katika tarafa tatu ambapo leo madiwani wa viti maalum Halmashauri hiyo wametembele na kutoa elimu hiyo kwenye kata ya Mwenge pamoja na kata ya Salawe zilizopo tarafa ya Nindo na kwamba tarafa hiyo inajumla ya kata 12.

Katika kata ya Mwenge baadhi ya wanachama wa CCM na jumuiya zake wamehudhuria kutoka kwenye vijiji mbalimbali ikiwemo Ipango, Mwenge, Zunzuli, Ihimbili, Mongozo pamoja na Ipango.

Kata ya Salawe imehudhuriwa na wanachama wa CCM na jumuiya zake kutoka vijiji vitano ikiwemo Azimio, Amani, Buduhe, Nzoza pamoja na kijiji cha Songambele.

Mwenyekiti wa madiwani viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambaye ni diwani wa viti maalum kata ya Lyamidati Mhe. Zawadi Lufungulo amehimiza wananchi wote kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura pamoja na daftari ya makazi ili kuwa na sifa za kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika badae Mwaka huu 2024.

Pia amewasisitiza wanawake wa UWT kujiamini na kuhakikisha wale wenye sifa wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  ikiwemo nafasi ya wenyeviti wa vijiji, mitaa pamoja na balozi.

Katibu wa madiwani  viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anastazia Robart Njile amezihimiza jumuiya za CCM ikiwemo UWT kuanza kuwatambua na kuwashawishi watu wenye sifa za uongozi wahakikishe wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali baada ya zoezi hilo kuanza.

Katibu wa umoja  wa wanawake UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magdalena Dodoma ametaja  baadhi ya sifa za mtu anayetaka kugombea nafasi ya uongozi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

“Sifa ya kwanza unatakiwa uwe mwanachama wa CCM hii ndiyo sifa ya kwanza yaw ewe kugombea katika Chama chetu cha CCM vile vile uwe mkweli na mwenye maadili mema usife mlevi kingine awe mstari wa mbele kuhudhuria vikao vya chama kwa mujibu wa katiba, awe anakubalika kwa dhati na watu kwahiyo tukachague viongozi wanaokubalika kwenye jamii, awe mpenda maendeleo na mbunifu, awe mwenye kuona mbali na aweze kusoma mazingira awe na maamuzi ya bila kuyumbishwa na mtu yoyote asiwe mwenye makundi ya kuchochea migogoro sifa nyingine mgombea wa CCM awe anajua kusoma na kuandika”.amesema Dodoma

Kwa upande wake diwani wa viti maalum kata ya Tinde Mhe. Helena Daud Mwanambuli pamoja na mambo mengine amekemea rushwa na ngono huku akiwasisitiza wanawake kutoa taarifa za watu watakaoomba rushwa ya ngono katika kipindi cha uchaguzi.

Nao baadhi ya madiwani wengine wa viti maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamewaomba wananchi kuendelea kuwaunga mkono viongozi waliopo madarakani wakiwemo madiwani wa kata, mbunge wa jimbo la Solwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hasa katika shughuli za maendeleo.

Malengo ya ziara hiyo ni kuhamasisha wanawake na wanachama wote wa CCM kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kuhamasisha wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, Usajili wa wanachama wa CCM na jumuiya zake pamoja na na kukemea Ukatili wa kijinsia.

Baadhi ya wanawake na wanachama wa CCM na jumuiya zake wamewapongeza madiwani wa viti maalum kwa kufanya ziara hiyo ambapo wameahidi kuzingatia yale yote ambayo wamekumbushwa iliwemo kuchua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Madiwani wa viti maalum Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga baada ya kuwasili katika kata ya Mwenge kwa ajili ya ziara yao.


 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post