LIGI YA MAKAMBA LAMECK (KRISMAS CUP) YAENDELEA, SALAWE FC WAIBUKA NA USHINDI DHIDI YA SOLWA FC


Na Mapuli Kitina Misalaba

Ligi ya Makamba Lameck maarufu kama Krismas Cup imeendelea kuchanja mbuga katika kata ya Salawe, ambapo leo Salawe FC wameibuka washindi wa mechi kali dhidi ya Solwa FC kwa ushindi wa goli moja.

Mfungaji wa goli pekee katika mechi hiyo ni Badala Masalu, aliyetikisa nyavu dakika ya 67, na kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa mechi (Man of the Match).

Mgeni rasmi wa mechi ya leo Disemba 2, 2024 ni mdau wa michezo Paul Daudi (MC Niache Kona), amepongeza kiwango cha juu cha ligi hiyo huku akitoa shukrani za dhati kwa Makamba Lameck kwa kuandaa mashindano ambayo amesema ni chachu ya kuwasaidia vijana kupata fursa za ajira kupitia michezo.

Wadau wengine wa michezo pia wameeleza kuridhishwa na ubora wa ligi hiyo, huku baadhi ya wananchi wakishukuru kufurahia mechi hizo bila kutozwa kiingilio.

Kwa upande wake, msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enick Kijida, ametangaza ratiba ya mechi inayofuata, ambapo kesho Beya FC watavaana na Ngubalu FC katika mchezo mwingine wa kusisimua.

Kumbuka ligi hii, imeandaliwa na Makamba Mussa Lameck kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka, ikiwa lengo ni kuibua vipaji vya michezo katika Mkoa wa Shinyanga na kuleta mshikamano wa kijamii.

Michezo hii, ambayo imeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kata ya Salawe na maeneo ya jirani, si tu burudani bali pia ni jukwaa muhimu la kuwaunganisha vijana na kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao wa kisoka.

Misalaba Media inakuletea taarifa za kina kuhusu michezo yote ya Ligi ya Makamba Lameck (Krismas Cup), ratiba, matokeo, na matukio ya nyuma ya pazia. Usiache kufuatilia kwa habari motomoto, mahojiano na wachezaji, na picha za kipekee kutoka viwanjani!

Mgeni rasmi wa mechi ya leo Disemba 2, 2024 ni mdau wa michezo Paul Daudi (MC Niache Kona), akipongeza ubora wa ligi hiyo ambayo inadhaminiwa na Makamba Lameck.

Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enick Kijida, akizungumza.

Msimamizi wa ligi hiyo, Mwalimu Emmanuel Enick Kijida, akizungumza.
Awali Salawe FC wakifanya mazoezi kabla ya mechi kuanza.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post