AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIJARIBU KUMPORA BABA PAROKO DAR

Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kufanya jaribio la kumpora Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Theresa iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi kampuni ya ulinzi ya Jatu, Jacob Mgwabati amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Septemba 6, 2019 saa 6 mchana wakati Padri huyo alipofika kanisani akitokea benki.

“Walipofika hapo wakambana paroko, alikuwa ametokea benki kulipa wafanyakazi, lakini hakuwa na hela. Wakamwambia tupe begi, wakati bado wanashangaa, wakatoa bastola mbili kila mmoja na bastola yake,” amesema Mgwabati.

“Paroko akaamua kuwapa begi, askari wetu akatumia busara, akaacha kwanza paroko asogee, walipoondoka akawatandika risasi, mmoja ikampata kwenye kiuno akaanguka, hakukaa sana akafa. Huyo mwingine alikimbia kwa miguu.”

Amesema baada ya tukio hilo polisi walioko karibu na kanisa hilo walifika na kumkagua mtu huyo na kumkuta na vitambulisho mbalimbali na leseni ya udereva na hirizi.
Via Mwananchi

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post