Mbunge Zaynabu Matitu Vullu akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Dimani Wilaya ya Kibiti
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani,Mh Zaynabu Matitu Vullu akikagua majengo ya Zahanati ya Dimani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa
Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi (UWT), Zaynabu
Matitu Vullu akiwaeleza Wanawake wa wilaya ya Kibiti juu ya Umuhimu wa
Bima ya Afya.
Na Mwandishiwetu
Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Pwani kupitia Umoja wa Wanawake wa chama Cha Mapinduzi
(UWT) ,Zaynabu Matitu Vullu amewaomba Wanawake wa wilaya ya Kibiti
kucheza Upatu wa kununulia bima za Afya na sio vyombo.
Mh Zaynabu amesema
hayo alipokuwa akizungumza na wanawake wa wilaya hiyo kwenye ziara yake
ya utekelezaji wa ilani ya CCM Kibiti.
“Mimi nawaomba
Wanawake wenzangu tuache kutunza vyombo badala yake tutunzane kadi za
CHF Iliyoboreshwa hili tuweze kupunguza gharama za matibabu pindi
tunapougua au kuuguliwa ndani ya familia” amesema Mh Zaynabu.
Amewaeleza kuwa Kama
Kila mmoja atauza kuku wawili nakujipatia bima kwa gharama ya Shilingi
30,000 ambayo itaweza kutibia watu sita ndani ya familia moja ambao Ni
Baba,Mama na wategemezi wanne.
Amesema matumizi ya
Bima yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini usiokuwa wa
lazima kwa kuokoa gharama za matibabu .
Aidha ametaja kuwa
matumizi ya Bima yanapunguza presha pindi Mama anapokuwa mjamzito pindi
unapofija wakati wa kujifungua kwa kusaidia kupata huduma kwa uhakika.
Pia aliwaomba
wamama hao kufikisha ujumbe huo kwa kinababa na waume zao kwani swala
la Afya ya familia ni jukumu la kila mmoja wetu.