Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe,akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wake na wadau wa kilimo.
Sehemu ya wadau wa kilimo wakifatilia mazungumzo yao dhidi ya Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein Bashe.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein
Bashe,akisisitiza jambo wakati wa Mkutano uliokutanisha wizara ya
Kilimo,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Fedha pamoja na wadau wa
kilimo hapa nchini.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Husein
Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha Sekta ya Kilimo
kuendelea kuwa na Matatizo, Migogoro na kesi za muda mrefu dhidi ya
Makampuni za Kilimo ambapo serikali imedhamiria kufuta kesi zote
zilizokuwa zinazikabili kampuni hizo ili ziweze kununua Mazao ya
wakulima. .
Mhe.Bashe amesema ameyasema hayo
Sept.3,2019 jijini Dodoma katika wa mkutano uliokutanisha wizara ya
Kilimo,Wizara ya Viwanda na biashara,Wizara ya Fedha pamoja na wadau wa
kilimo hapa nchini.
Naibu Waziri Bashe amesema
kampuni za kilimo zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh.Trilioni 10 na
Serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma
kwa wakulima hivyo serikali ina mkakati kabambe wa kufuta kesi na faini
zote hizo ili ziweze kutoa huduma kwa wakulima.
Aidha,Mhe.Bashe amesema
wamekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania[TRA] kuwa ndani ya siku 90
Kuanzia leo Sept.4,2019 suala la madai kwa kwa Kampuni 4 za kilimo
litakuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.
Pia Naibu Waziri Bashe amesema
kuna zaidi ya kilo Mil.12 za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na
Kampuni za kilimo chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania zitakutana na
wakulima kununua kilo hizo kuanzia Sept.12,2019 .
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi
ya Tumbaku ,Tanzania Tobacco Board[TTB] Hassan Mwakasuvi amesema
kuwa ni vyema wakulima kuheshimu mikataba huku akisema kuwa maazimio ya
kikao hicho ni Faraja kwa wakulima katika msimu ujao wa kilimo.
Naye Mwenyekiti wa vyama vikuu
vya wakulima wa Tumbaku Tanzania Emanuel Cherehani ameishukuru serikali
kwa maamuzi hayo huku akiomba kuanza kutekelezwa ndani ya Muda husika
uliotajwa ili isiathiri zaidi wakulima huku akiwaomba wakulima kuendelea
kutunza mazao yao ya tumbaku.
Aidha,Cherehani amesema hapo awali
uzalishaji wa zao la tumbaku kwa mwaka 2015 ilikuwa milioni 120 lakini
umeshuka mpaka milioni 41 jambo ambalo limeathiri kwa wakulima na
Serikali kwa Ujumla.