BREAKING NEWS: Mahakama Afrika Kusini yaiachia Ndege ya Air Tanzania Iliyokuwa Inashikiliwa

Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja na mlalamikaji alipe gharama za kesi

Ndege hiyo tayari ipo njiani kurejea nchini ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg.
Waziri wa Ujenzi, Injinia Isack Kamwelwe aliutangazia umma mbele ya Rais Dkt John Magufuli alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa bodi ya wahandisi, wajenzi na wakadiriaji wa majengo nchini

Amesema ndege hiyo iko kwenye taratibu za kuirejesha nchini ndege hiyo na kwamba safari za ndege hiyo zitaendelea kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

Amesema suala hilo ambalo limeleta taharuki kubwa miongoni mwa Watanzania sasa litaendelea na shughuli zake na kuwataka watanzania kuendelea kuitumia ndege hiyo kwenye safari zao na kwamba huduma zitaendelea kutolewa kama kawaida kwa ubora wa hali ya juu.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post