Abiria
waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Kimotco kutoka Arusha
kwenda Musoma mkoani Mara wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha
njia na kupinduka eneo kati ya Itilima na Maswa mkoani Simiyu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, William Mkonda amesema ajali hiyo imetokea jana Alhamisi Septemba 5, 2019 saa 12 jioni.
"Hakuna vifo kuna majeruhi ambao bado hawajafahamika na wanapatiwa
matibabu katika hospitali ya Maswa. Tunasubiri taarifa ya madaktari wa
Maswa ili tutoe taarifa kwa umma,” amesema Kamanda huyo.