Mchungaji Brighton Samajomba kutoka
nchini Zambia, amefariki dunia kwa kinachotajwa kupatwa na Utapiamlo'
akiwa katika mfungo ambao alikuwa anadhamiria kufikisha siku 30.
Mpaka anafariki mchungaji huyo alikuwa amefikisha siku 20 hivyo zilikuwa
zimebaki siku 10 tu kutimia siku 30, Kaka wa Marehemu Reagan Samajomba
anasema ndugu yake alikuwa na kawaida ya kufunga na kufanya maombi kwa
muda mrefu kuliko wengine.
Katika mfungo wa siku 30 Kaka wa Marehemu anasimulia kuwa ndugu yake
aliamua kufanya hivyo huku lengo kuu likiwa kuiombea familia yake pamoja
na waumini wa kanisa analoliongoza mshikamano pamoja na umoja uzidi
kuimarika.
"Jambo jema alilotuachia sisi kama familia ni namna alivyofariki sababu alikuwa karibu na Mungu," alisema Kaka wa Marehemu.