Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. John Pombe Magufuli
ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert
Mugabe ambaye ameaga dunia nchini Singapore alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Magufuli
kupitia akaunti yake ya Twitter amemwelezea Mugabe kuwa alikuwa
kiongozi shupavu, jasiri ambaye aliupinga na kuukataa ukoloni kwa
vitendo.
"Afrika imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina."