Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu
Jerry Muro kwa kushirikiana na Taasisi ya walemavu wa Uti wa mgongo KASI
imetoa misaada mbalimbali kwa walemavu wenye matatizo ya Uti wa Mgongo
walioko katika wilaya ya Arumeru.
Dc Muro ambae ameamua kuonyesha
juhudi binafsi katika kuwasaidia watu wenye ulemavu amesema wametoa
misaada ya kuanza maisha ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu ili
waweze kumudu maisha hatua itakayowasaidia kuwaondoa katika kundi la
utegemezi katika familia jambo linalochangia watu kuwanyanyapa.
Misaada iliyotolewa ni vifaa vya
kuanzisha biashara ya vifaa vya ujenzi, maji kwa ajili ya mradi wa kuuza
maji ya jumla , vifaa vya majumbani zikiwemo chupa za chai , hotpot,
mamia ya kuku wa kienyeji kwa ajili ya bishara ya mifugo, mbuzi pamoja
na bidhaa mbalimbali.
Wakizungumza mara baada ya Dc
Muro kukabidhi misaada hiyo, kiongozi wa jumuiya ya watu wenye ulemavu
wa uti wa mgongo kwa mikoa ya kilimanjaro na Arusha (KASI), Deogratius Chami ameipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe,
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuwajali watu wenye ulemavu
hatua inayowasaidia kuwajengea uwezo wa kupambana na changamoto
walizonazo ambapi amesema wao kama KASI wanapambana kuwafikia walemavu
wengi zaidi katika ukanda wa kaskazini
Kwa upande wao viongozi wa chama
cha mapinduzi CCM wilaya ya kichama ya Meru wakiongozwa na katibu
mwenezi Comrade Joshua Hungura wamesema jitihada zinaonyeshwa na mkuu wa
wilaya ya Arumeru katika kuyafikia makundi mbalimbali yenye mahitaji
maalum ni kielelezo tosha cha utekelezaji wa ilani ya chama cha
mapinduzi katika kuwahudumia watu wenye ulemavu