IGP SIRRO ASEMA UHALIFU, TISHIO LA KIUSALAMA BADO NI TATIZO KUBWA UKANDA WA MASHARIKI MWA AFRIKA




Na Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amesema kuwa bado ukanda wa Mashariki mwa Afrika unakabiliwa na matishio ya kiusalama ambayo ni usafirishaji haramu wa binadamu, utoroshwaji wa madini,ujangili na makosa ya kimtandao, makosa ambayo wahalifu wa kimataifa hutumia kutengeneza fedha kwaajili ya kuendelea kufanya  makosa makubwa zadi hasa ya ugaidi.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi (EAPCCO) leo kinachoendelea Jijini Arusha ambapo  (IGP)  Sirro amesema matukio ya kigaidi yanatokea maeneo mbalimbali duniani ni kiashiria tosha kuwa kuwa nchi Bara la Afrika bado haziko salama

“Kama mnavyojua yamekuwepo matukio ya aina hiyo katika Nchi nyingi duniani na kwa upande wa bara la Afrika baadhi ya mataifa yamekuwa wahanga wa matukio haya zikiwemo nchi za Nigeria,Algeria,Somalia,Msumbuji ,Kenya n.k.’’Alisema IGP

Amesema kumekuwepo kwa matukio ya aina mbalimbali katika nchi  nyingi Duniani na kwa upande wa Bara la Afrika baadhi ya mataifa yamekuwa wahanga wa matukio hayo ikiwemo nchi za Nigeria, Algeria, Somalia, Msumbiji na Kenya.

Amesema japokuwa kwa sasa inaonyesha kunautulivu lakini taarifa za kiitelejensia zinaonyesha kuwa matishio ya vikundi vya ugaidi bado yapo na yanaendelea kujiimarisha na kufungua seli maeneo mbalimbali ndani na nje ya mpaka

“Magaidi kila siku wanatafuta mianya ya kufanya matukio  ya kigaidi ili kujitapa huku wakitaka kuimarisha dunia kuwa wapo na wap imara ,hivyo hakuna nchi iliyo salama lazima kuwe na uwezo wa kubaini na kuzuia matukio haya

Amewataka wakuu hao kuhakikisha wanabuni mikakati ya utendaji na utatuzi wa changamoto za uhalifu  wa kimtandao (Cyber Crimes) yanayotokana na mabadiliko ya kukua kwa teknilojia ya habari na mawasiliano ikiwemo uboreshaji wa oparesheni zao sambamba na kukusanya uchakataji wa taarifa za kiitelejensia.

Awali  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini, Robert Boaz alisema nchi 13 zimeshiriki mkkutano huo kasoro nchi ya Comoro na kusisitiza kuwa wataalam hao watajadiliana mbinu mbalimbali kwa kutumia teknolojia kwaajili ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Uratibu ya EAPCCO na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Sudani,Gedion Kimilu amesema kuwa anatambua kazi kubwa inayofanywa na shirikisho hilo ya
kupambana na vitendo mbalimbali vya uhalifu haswa Ugaidi na kuwahisi wajumbe hao kuendelea kuwa na mikakati ya pamoja ya kiitelejensia ya kupambana na uhalifu kwani uhalifu mwingi unafanywa kwa mbinu za kiteknolojia.

Pia watajikita zaidi katika mbinu za kuongeza ushirikiano na kukabilia na mbinu za uhalifu ikiwa ni pamoja na kubadilishana watuhumiwa sambamba na kufanya oparesheni za pamoja katika kuleta matokeo chanya.

Aidha Jeshi la polisi Tanzania ambalo linaenda kuwa mwenyekiti wa EAPPCO kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao limeahidi kuendeleza ushirikiano na nchi wananchama kwa wote katika kuhakikisha eneo lao linakuwa mahali salama pa kuishi,sambamba kwa kushirikiana na INTERPOL makao makuu na Ofisi za INTERPOL za Nairobi kuwa watendelea kubaki wamoja kwa lengo la kuvumbua mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu na wahalifu wabainike mapema,ili wakamatwe kabla hawajatekeleza nia yao.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post