Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe akiongea katika katika maafali ya 11 ya kidato cha nne pamoja na maafali ya 17 ya darasa la saba yaliofanyika katika viwanja Wa shule hiyo vilivyoko katika kijiji Olosiva
Wanafunzi wa kidato cha nne wakicheza wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao
wanafunzi wa chekechea wakicheza ngoma kwa ajili ya kuwaaga kaka zao na dada zao wanaoitimu elimu yao ya msingi pamoja na sekondari
Afisa utawala Wa shuleza Trust st.Patrick schools Dinna Patick Khanya akiongea katika mahafali hayo
mkurugenzi mkuu wa shule ya Trust St Patrick schools Patrick Thomas Khanya alisema kuwa jumla ya wanafunzi 76 wamehitimu darasa la saba ,huku wanafunzi 41 wakihitimu kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo
Wanafunzi wa darasa la saba wakicheza mbale ya mgeni rasmi wakati wakiimba wimbo wa kuwaaga wadogo zao
Na
Woinde Shizza, APC BLOG, ARUSHA
Imebainika kuwa
ugomvi Wa familia majumbani hususani wazazi unachangia kwa kiasi kikubwa
baadhi ya watoto kushindwa kufanya vizuri
kwenye masomo, na muda mungine kusababisha kufeli kwa masomo yao
shuleni.
Hayo yamebainishwa
na Afisa utawala wa shule za Trust st.Patrick schools Dinna Patick Khanya katika maafali ya 11 ya kidato cha nne pamoja na maafali ya 17 ya darasa la saba yaliofanyika
katika viwanja Wa shule hiyo vilivyoko katika kijiji Olosiva ndani ya halmashauri ya Arusha
wilayani Arumeru ambapo alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi
wanaofeli darasani ,ni kutokana na ugomvi wawazazi majumbami.
Aidha pia amesema kuwa wazazi
wengi wamekuwa hawana tabia ya kukaa na watoto wao na kuongea kuhusiana na
mambo mbalimbali yanayowahusu pamoja na kuwaeleza namna dunia inavyoenda ,
kuwaeleza mambo mabaya yaliopo duniani.
Alisema baadhi matatizo ya ugomvi wa familia
yanachangia kwa kiasi kikubwa kuwaadhiri watoto haswa wawapo masomoni kwani mda
mungine wanashidwa kuwa makini darasani
kutokana na kuathirika kisaikolojia
kutokana na ugomvi wa wazazi
Alibainisha kuwa kumekuwa na ongezeko la
wazazi wenzi kugombana majumbani na kufikia hatua ya kuwaonyesha watoto wao
tofauti zao kitu ambacho sio kizuri kwani unapo muonyesha mtoto tofauti zenu
wazazi ,mnawafanya waathirike na wakati mwingine badala ya kusoma wanawaza namna wazazi wanavyogombana .
“wazazi
wengi sasa hivi wamekuwa wababe mnagombana kila mmoja anataka kuonyesha
ubabe wake mbele ya mtoto mkizani mnajenga lakini mnabomoa ,kwani kwanza
mnamuumiza mtoto kisaikolojia ,mnamuonyesha mtoto maadili mabaya ,na tabia
mbaya pia mnamfanya mtoto badala asome anaanza kuwawaza, nimeona hapa shuleni
kuna watoto wanamaliza leo darasa la saba lakini kutokana na tabia za wazazi wao
hawatamani hata kuondoka shule , wanafikia hatua yakusema mwalimu mimi bora
nibaki hapa hapa shule maana nyumba hapafai kitu ambacho sio kizuri na
kinawaumiza sana “alisema Dinnah
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya
Arumeru Jerry Muro, Mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe aliipongeza shule
hiyo kwa kuwalea watoto katika maadili mazuri na kuwapa elimu mbalimbali
ikiwemo ya kidini ,kimwili na kitaaluma ,ambapo pia alitumia muda huo
kuwasisitiza wazazi kuendelea kuwapa watoto hao waliohitimu msingi mzuri wa kuendeleza vyema yale yote
waliofundishwa wakiwepo shuleni,.
Aliwasihi wazazi kutengeneza upendo wa kweli
na wanapokuwa na kasoro zao kutowashirikisha watoto kwani wanapowashirikisha wanaweza kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya
kisaikolojia ambayo huathiri uwezo wao wa kujifunza shuleni.
“wazazi mafanikio ya manafunzi ya kielimu na
kimaisha yamegawanyika kwa misingi mitatu ambayo msingi wa kwanza wa kumjenga
mwanafunzi ni pale shuleni ambapo
anaposoma ambapo walimu wanamlea kwa asilimia 30,msingi wa pili ni mwanafunzi
mwenyewe ambaye yeye anachangia kwa asilimia 30, na asilimia 40 ambayo imebaki ni ya mzazi sasa hapa mzazi usipo
fanya vyema kwa asilimia 100 inakuwa
umemuharibia mtoto maisha kiujumla hivyo ni jukumu la kila mzazi
kuhakikisha anafanya vyema katika suala
la asilimia yake ili mtoto asifeli”alisema Mwaisumbe
Alimalizia kwa kuwataka wazazi kujenga tabia
ya kufuatilia watoto wao mashuleni ili
kujua maendeleo yao shuleni na sio kuwaachia walimu tu kwani wanapowaachia
walimu wanawapa mzigo mkubwa .
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shule ya Trust St Patrick schools Patrick Thomas Khanya
alisema kuwa jumla ya wanafunzi 76 wamehitimu darasa la saba ,huku wanafunzi 41 wakihitimu kidato cha nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo
Aliwataka wanafunzi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili waweze
kujitegemea wenyewe na sio kutegemea wazazi ,huku akiwataka wazazi kuwapa
watoto miongozo wa kimaisha maana bado
ni wadogo na wanaitaji malezi yao mema ,Aidha aliwaonya wanafunzi hao kutojiingiza katika masuala ya siasa
badala yake watilie mkazo katika elimu waliopewa na ambayo wataipata wakati
wakijiendeleza.