Jamii
Mkoani Kagera imetakiwa kutoa ushiriakiano katika idara ya uhamiaji ili
kuweza kuwabaini wananchi wanaoingia nchini pasipo kufuata taratibu na
sheria zinazoitajika.
Hayo
yamesemwa na Afsa uhamiaji mkoa wa Kagera Bwana Christopher Pendo
wakati akizungumza na mpekuzi blog ofisini kwake katika kuelekea kwenye
ushaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka
huu.
Bwana
Christopher ameongeza kuwa idara ya uhamiaji mkoa imejipanga vyema
kuhakikisha wananchi watakaochiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
ni raia wa Tanzania na kuwataka wananchi kuwaripoti mara moja katika
idara ya uhamiaji wale wote watakao washuku kuhusu uraia wao.
Ameongeza
kuwa kwa sasa wanaendelea na utaratibu wa kuwabaini walowezi wanaoishi
katika mkoa huo ili kubaini idadi yao na badae utaratibu utafanyika ili
kuwapa kibari cha kuishi kama raia wa Tanzania.
Bwana
Christopher amewakumbusha wananchi kutokubari kutoa wala kupokea rushwa
kwani ni kosa la jinai na mtu yoyote atakaye bainika sheria itachukua
mkondo wake.